Mkurungezi
Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti
205 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat, Safia
Rijal kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo
chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo
imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Mkurungezi
Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti
205,Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat, Safia
Rijal, kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo
chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo
imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Mkurungezi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi, Safia Rijal akikabidhi moja ya meza na viti kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi za Kijiji cha Kijini Maatemwe na Wawakilishi wa International Volunteers Oman Hemed Mohammad, Danny Kim na Nahya Khamis wa Mradi wa Best Of Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A, Unguja.
Mkurungezi
Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson akiwa na Mwakilishi wa Internalional Volunteers Oman Danny Kim, wamekali meza na viti walivyokabidhi kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja, kulia Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalazi, Safi Rijal na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kijini Matemwe Mwalimu Ulimwengu Mkadam. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Kijini.
Mwakilishi wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar Mohammed Issa akitowa maelezo kabla ya hafla ya makabidhiano wa vifaa kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.
Mwakilishi wa International Volunteers Oman Danny Kim akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205, kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja Skuli hizo zinapata ufadhili kupitia Mradi wa Bset of Zanzibar, uliooko chini ya Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar, inayojenga kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibar. Safia Rijal akizungumza wakati wa hafla hiyoya kukabidhiwa Viti na Meza 205 kutoka kwa Mradi wa Best of Zanzibar kwa kushirikiana na Internalional Volunteers Oman, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.na kuhudhuriwa na Wananchi wa kijiji hicho.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekongari na Msini Kijini Matemwe Mwalimu Ulimwengu Mkadam akitowa neno la shukrani kwa msaada huo na kusema umefika wakati muwafaka.
Wazee wa Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Meza na Viti vyake 205 kwa ajili ya matumizi ya Skuli ya Sekondari na Msini Kijini Matemwe, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Kijini.
Mkurungezi
Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson, akiwasalimia Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kijini baada ya hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibar, Safia
Rijal kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo
chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo
imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Pennyroyal Limited kupitia kitengo
chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar wakishirikiana na International
Volunteers kutoka Oman wametoa msaada wa madawati 200 yenye thamani ya Tsh
18,000,000/- ( Shilingi millioni kumi na nane).
Akiongea katika sherehe za
kukabidhiana, Mkurungezi Mkuu Bw. Brian Thomson alikua na haya ya kusema:
“Best of Zanzibar imejitolea
kuboresha elimu katika shule za Kijini na Mbuyu Tende. Tumejiwekeza katika
progamu tofauti za kielimu katika shule hizi mbili zikiwemu Masomo ya ziada
(After Hours Tutoring program) kwa wanafunzi 500, na kuwasomesha walimu 30 masomo ya lunga ya
Kingereza na mbinu za kufundishia ili kuongeza uwezo na ujuzi wa walimu hao.
Tunawashukuru sana
International Volunteers kwa moyo wao wa kujitolea na kushirikiana nasi
katika kutoa huduma kwa mashule.”
Mkurungenzi
huyo alisisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii na ukuwaji wa uchumi
wa nchi, ndio maana Best of Zanzibar
imejikita katika uboreshaji wa elimu Zanzibar.
“Nia
yetu kuu ni kuleta manufaa na kuedeleza msingi mzuri wa kiuchumi Zanzibar.
Kwa muda mrefu sana watoto wa shule ya msingi Kijini na Mbuyu Tende wamekaa
chini bila madawati kuwaletea ugumu katika kuelewa masomo na kupunguza
ufanisi wao wa masomo.
Best of Zanzibar inashirikiana kwa ukaribu na Wizara
ya Elimu katika kuboresha viwango vya elimu katika shule za Kijini na Mbuyu
Tende. Na tunaishukuru sana Wizara ya Elimu kwa kutuunga mkono katika program
zetu.” Aliongezea, Brian Thomson.
Shule
ya Kijini ina wanafunzi 903 na Mbuyu Tende inawanafunzi 603, katika wanafunzi
hao 353 wanakaa chini bila madawati.
Mkurungezi
wa Masomo ya Pre-Msingi na Msingi Wizara ya Elimu, Safia Rajil alikua
katika hafla hiyo na alipongeza
wawekezaji hao kwa msaada wao.
“Kwa niaba ya Wizara ya Elimu napenda
kutanguliza shukurani zetu za dhati kwa Best of Zanzibar na International
Volunteers kwa kutoa madawati haya kwa shule hizi mbili. Msaasa huu utaleta
madadiliko nakuongeza ufanisi wa watoto.”
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Kijini, Ulimwengu Mkada Makame alishukuru sana kampuni ya
Pennyroyal Ltd kwa msaada wao.
“ Shule
yetu ilikua haina madawati kwa muda mrefu sana, tunashukuru Best of Zanzibar
kwa kutukumbuka shule yetu.”
|
No comments:
Post a Comment