NSSF
TANGAZO
Monday, May 20, 2013
WAZIRI WA MAMBO YA NJE BERNARD MEMBE AKUTANA NA MABALOZI JIJINI DAR ES SALAAM.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe
akiongea na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania leo
jijini Dar es salaam alipokutana nao kujadili maandalizi ya mkutano wa
Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) na
mchango wao katika kuhamasisha ushiriki wa nchi wanazotoka katika
mkutano huo utakaofanyika mwezi ujao. Kushoto kwake ni Balozi wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo Juma - Alfani Mpango.
Meneja Mradi wa maandalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano
kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi
kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao kuhusu maendeleo na maandalizi
ya mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika mwezi June jijini Dar es
salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais 10 kutoka
nchi zilizoendelea.
Sehemu ya mabalozi wakifuatilia hatua mbalimbali za maandalizi ya
mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart
Pertinership) na mchango wao katika kuhamasisha ushiriki wa nchi
wanazotoka katika mkutano huo. Zaidi ya washiriki 500 wanatarajiwa
kwenye mkutano huo utakaojadili kwa kina matumizi ya Sayansi na
Teknolojia katika kuleta Maendeleo kwa nchi zinazoendelea.

Meneja Mradi wa mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya
Wote (Smart Pertinership) Rosemary Jairo,(kushoto mbele aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwa mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao jijini Dar es salaam kuhusu maendeleo na
maandalizi ya mkutano huo utakaohudhuriwa na wachumi, wanasayansi na
viongozi mbalimbali wa serikali kutoka ndani na nje ya nchi.(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO).
No comments:
Post a Comment