Waziri wa fedha, Dk, William Mgimwa,(kushoto) akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Mark Wiessing.
Mheshimiwa waziri wa fedha, Dk, William Mgimwa akichukuliwa alama zavidole na Ofisa mauzo ya Nje
NMB, Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki
mkoani Dodoma.
Benki ya NMB
imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbalimbali za kibenki,
ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini
Tanzania. Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua akaunti ya
Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha ndani ya dakika kumi
·
Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap
Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:
· -
Kuona salio la akaunti yako popote ulipo
· -
Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa
· . .
Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
· .
Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
· .
Kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye
ATM.
No comments:
Post a Comment