Benki ya
NMB imefadhili maonyesho ya ubunifu wa
watoto waliokusanywa na Tanzania Mitindo House. Maonyesho ambayo yatahusisha
shughuli mbali mbali za kazi za mikono ambazo watoto wenye vipaji wamekua
wakizifanya. Maonyesho haya yataanza
tarehe 8 Juni hadi tarehe 9 juni 2013
kuanzia saa 9 hadi saa 2 usiku pale Tanzania Mitindo House. Kwa msaada wa benki
ya NMB, watoto hawa watauza kazi zao na kujipatia fedha ambazo zitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za NMB.
Fedha hizi zitawasaidia watoto hawa katika kuendeleza maisha yao ya kila siku
hasa kielimu.
Tanzania
Mitindo House ni Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imedhamiria kukusanya na
kuendeleza Vipaji vya watoto yatima
ambavyo vingedidimia bila msaada wowote.
Mtoto Frank kutoka nyumba ya watoto Yatima Tanzania Mitindo
House akionyesha umahiri wa kuchanganya rangi katika michoro tofauti
tofauti.Frank anauwezo wa kuona lakini hana uwezo wa kusikia vizuri ni mtoto
mwenye kipaji ajabu.
Mtoto Ahmed kutoka shule ya wasiosikia Buguruni kutoka nyumba ya watoto Yatima Tanzania Mitindo
House akionyesha ubunifu wa kazi yake wakati wa masomo ya kazi za mikono.
No comments:
Post a Comment