Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Denise Nkurunziza, Mke wa Rais wa Burundi wakati wa sherehe za kupokea tuzo zilizofanyika huko New York nchini Marekani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Equatorial Guinea, Mama Dona Constancia Mangue de Obiang wakati wa hafla ya kupokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Award 2013 inayotolewa na Shirika la Voices of African Mother’s la nchini Marekan
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia na NGO Representative to United Nations for the International Association of Applied Psychology and the World Council of Psychotherapy wakati wa utoaji tuzo kwa Wake wa Marais na wanawake waliofanya vizuri barani Africa katika kutekeleza malengo ya millennia. Sherehe hizo zilifanyika huko New York nchini Maraekani.
Baadhi ya watu waliofuatana na msafara wa Mama Salma Kikwete pamoja na uongozi na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Mheshimiwa Balozi Tuvako Manongi wakishiriki katika shamrashamra za kukabidhiwa tuzo kwa Mama Salma Kikwete huko New York.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Awards,2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science, Cultural and Health Advancement Foundation la nchini Marekani. Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto waliokosa fursa na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo hiyo Katibu wa WAMA Foundation , Ndugu Daud Nassib wakati wa kupokea tuzo hiyo huko New York nchini Marekani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia waalikwa waliohudhuria sherehe za utoaji tuzo kwa wake wa Marais wa Bara la afrika zilizofanyika huko New York nchini Marekani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa na Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuoi Kikuu cha Columbia mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo yake.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana rasmi na Mwanzilishi na Rais wa Voices of African Mother’s Inc Mrs Nana- Fosu Randall, ambaye shirika lake ndilo lililotoa tuzo kwa wake wa Marais wa Afrika waliotimiza baadhi ya malengo ya millennia.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment