KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Monday, July 29, 2013

UKAME WA MVUA KATIKA VIJIJI VYA MANGESANI,KISONGO,LIHIMALYAO,LUYAYA NA NAMAKONGORO WILAYANI KILWA MKOA WA LINDI WASABABISHA HALI MBAYA YA MAJI NA CHAKULA.

 Eneo la Mto Matanda lililokuwa likihifadhi maji limekauka kama inavyoonekana vyufa katika ardhi hiyo.
 Eneo la visima vilivyokuwa vipatikana maji katika Kijiji cha Luyaya limekauka na kukimbiwa na Wananchi.
 Shamba la muhogo ambao umekauka na jua kali katika barabara ya Namakongoro kutoka Lihimalyao.
Watoto wa Kijiji cha Namakongoro wakitoka kuchota maji katika Pango lenye urefu wa mita 50 kutoka usawa wa ardhi,ambapo watoto kama hawa hawaruhusiwi kuingia katika Pango hilo lililotumika kujificha wazee waliopigana wakati wa Vita vya Majimaji.
Dogo akielekea katika Pango la Ng'ongoro ili apate msaada wa kuchotewa maji na kurudi nayo Kijijini Namakongoro.
Mama mkazi wa Kijiji cha Namakongoro akiibuka katika Pango la Ng'ongoro akiwa na ndoo ya maji kichwani huku akishikilia nguzo zinazoingia katika Pango hilo.
Hili ni Tundu la Pango la Ng'ongoro sehemu ya juu limezungukwa na mawe hadi chini ambako kuna nafasi kubwa ya kama kiwanja cha nyumba kubwa chini ya ardhi.


  Watoto na wakijitwisha ndoo na wengine wakiwa tayari kuelekea nyumbani Kijijini Namakongoro.
 Dogo akirudi nyumbani baada ya kupata maji.
 
 Kina mama wakichota maji ndani ya Pango la Ng'ongoro lenye urefu wa mita 50 kutoka juu ya ardhi.

Wananchi wa Kijiji cha Namakongoro Kata ya Lihimalyao Tarafa ya Pande Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi wakiingia ndani ya Pango la Ng'ongoro tayari kuchota maji yenye Chumvi kwa kiasi kikubwa lakini kwa matatizo ya maji waliyonayo hayo yanawafaa kwa shida.

TAARIFA FUPI
Vijiji hivyo vilivyotajwa hapo juu ya kichwa cha habari vimekumbwa na ukame mkubwa sana na kupelekea kuwa na wakati mgumu katika maisha yao.

Watanzania,Serikali,Mashirika ya Umma,Mashirika ya Kimataifa na wenye moyo wa huruma tembeleeni Vijiji hivyo ili muone majanga wanayokabiliana nayo Watanzania wezenu ambao wanahitaji msaada wa hali na mali katika kipindi hiki kigumu kwao.

TANZANIA LIVE BLOG,  Itaendelea kutoa picha zaidi za matukio ya matatizo ya maji fuatilia uone matatizo yanayowakabili wakazi wa Kanda hii ya Pwani ya Bahari ya Hindi Kusini kati ya Tanzania Kilwa.

No comments: