KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, August 16, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAOMBOLEZA KIFO CHA KATIBU MKUU IKULU MSTAAFU ABEL MWAISUMO.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay  Dar es Salaam.
Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo huku Mama Salma Kikwete akisubiri zamu yake wakati walipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki juzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Mama Salma Kikwete akifariji wafiwa wakati yeye na Rais Kikwete walipokwenda kuomboleza na kutoa pole kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo,aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiomboleza na kufariji wafiwa  katika  msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu, Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam>(PICHA NA IKULU).

No comments: