Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina pamoja na wazazi wa mbunge huyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri
husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa
kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za
wananchi mitaji na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri
lazima wachukue jukumu la moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi,
alisema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu
wa hifadhi ya Maswa kupita kiasi, alisema sheria zingine ziangalia
wakati zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema
zikarekebishwa.




No comments:
Post a Comment