Wanachama wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa Temeke, Joseph Yonah(shati nyeusi) na wanachama wengine na baadhi ya viongozi ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa Dar es Salaam.
Wakiwa na Mabango yao.
Ofisa wa Polisi akiwaambia wafuate utaratibu katika Ofisi za mhasibu Mkuu wa Serikali.
Polisi akiwataka kutawanyika.
Ofisa wa Polisi akiwaambia jambo.
Wakizungumza na naibu Msajili wa Vyama,Sisty Leonard Nyahoza (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wao wa Temeke, Joseph Yonah.
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU WAJUMBE WA BARAZA KUU NA
MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWENDA KWA
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA NA KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA
SERIKALI.
A.UTANGULIZI
Ndugu wanaHabari,
Mtakumbuka kwamba Juzi, katibu wa
CHADEMA mkoa wa Tabora kwa niaba yetu wajumbe 78 wa baraza kuu na viongozi wengine wa mabaraza ya vijana na
wanawake 4 kufanya kuwa jumla ya
wajumbe 82 kwa pamoja tulizungumza
na waandishi wa habari kuzungumzia maswala mbali mbali yanayotishia ustawi wa
chama chetu.
Na mtakumbuka kwamba tuliazimia
kwamba tutakwenda kumuona msajiri wa vyama vya siasa ili tumpatiemalalamiko
yetu haya.
B. KWENDA KWA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA.
Ndugu wanaHabari, Mapema leo
Tumekwenda ofisini kwa msajiri wa vyama vya siasa na tumekabidhi barua yenye malalaiko
mbali mbali juu ya uvunjifu ya KATIBA unaofanywa kihuni na kwa makusudi na
viongozi wetu wa CHADEMA hasa mwenyekiti Mbowe na Katibu mkuu SLAA.
Tunaambatanisha na nakala ya barua tuliyoipeleka kwa msajiri.
C. KWENDA KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.
Ndugu wanaHabari, Kutokana na Ukweli
kwamba viongozi wetu hasa Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu SAA, wanahusika moja
kwa moja na Ubadhirifu wa fedha za chama zinazotokana na kodi za Umma, za zaidi
ya BILIONI 10.038 na wao wanasema hayo madai siyo mapya na kwamba wameyazoea.
Hivyo basi tumepeleka kwa mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, barua yenye kuomba kupatiwa nakala ya
Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu za CHADEMA baada ya ofisi yake kukamilisha ukaguzi
huo.
Pia pamoja na kuomba Nakala hiyo,
tumeomba pia mkaguzi azitoe taarifa hizo hadharani ili wanachama wa CHADEMA na
watanzania kwa ujumla waone kilichopo ndani yake.
D. MSINGI WA HOJA ZETU.
Tunamuomba katibu mkuu wa chama,
ajibu hoja zetu na aache kuleta viroja kama ambavyo amenukuliwa na vyombo vya
hbari jana.
Msingi wa hoja zetu sisi ni katibu
mkuu kujilip zaidi ya million 130 kwa mwaka huku makatibu wake wa mikoa, wilaya
na kata wakilipwa shilingi 0
Msingi wa hoja zetu ni katibu mkuu
SLAA kujikopesha zaidi ya Millioni 160 kwenda kumalizia deni la nyumba yake
bila kufuata utaratibu wowote wa kukopa
Msingi wa hoja zetu ni kitendo cha
mbowe kutukodishia magari yake kwa mamillioni ya pesa kila tunapotumia, halafu
yanapokuwa chakavu anatuuzia FUSSO MBILI chakavu kwa million 600
Msingi wa hoja zetu ni kitendo cha
MBOWE kukiuzia chama VX V8 MBILI ambazo amenunua kwa pesa za chama halafu
anazisajiri kwa jina la MBOWE HOTELS.
Hiyo ndio misingi ya hoja zetu, Slaa
alitakiwa kujibu hoja hoja hizi, aeleze ni kwanini anatumia vibaya pesa za umma
hata kabla hajaingia madarakani, SLAA aeleze kama leo tupo wapinzani tunachezea
katiba hivi, je tukiingia madarakani tutakuwaje?.
SLAA aeleze kama sisi viongozi wake
wa wilaya ni WAJINGA, nay eye ndio katibu mkuu wetu, sasa je yeye ni KUBWA
JINGA?, AU MJINGA MKUU?, AU ZEZETA?. Unawezaje kukaa na viongozi WAJINGA,
ukawaomba ushauri, ukawatumia halafu wakikusoa ndio ukawajua kuwa WAJINGA, je
SLAA sio MJINGA ZAIDI YETU?.
E. KUHUSU KUWAKANA WAJUMBE NA
WANACHADEMA.
Ni vema mkatambua kuwa viongozi wakuu
wa CHADEMA wanakimbilia Kuwakana wanachama na viongozi wake pindi linapotokea
swala bila kujibu vilivyopo ndani ya swala hilo, jana wamemkana JOSEPH YONAH
ambaye ni mwenyekiti halali wa CHADEMA wilaya ya temeke kiasi cha mwanzoni mwa
mwaka huu KUMTEKA NA KUMTESA.
Lakini pia huu hapa ni mwendelezo wa
tabia ya CHADEMA KUWAKANA VIONGOZI WAO NA MATENDO YAO.
·
Alipouwawa
CHACHA WANGWE, na ilipotangazwa kwamba wakati anauwawa alikuwa na ndugu DEUS
MALLYA ambaye ni mwanaChama wa CHADEMA kwenye Gari, asubuhi yake, Ndugu John
Mnyika, alimkana na kusema hamtambui na kwamba serikali iseme DEUS MALLYA NI
NANI na anatokea wapi?, na mambo mengineyo, na DEUS MALLYA naye akajidai
hamjui, alipotoka GEREZANI akamuomba msamaha kwa kumkana.
·
Alipojihudhuru
uenyekiti wa Mkoa wa SINGIDA muasisi wa CHADEMA mkoani Humo, ndugu Wilfred
Kitundu, Chadema badala ya kujibu hoja zake Walimkana
·
Alipojiondoa
chamani katibu wa sekretariety na muajiriwa wa chama ambaye pia ni mwenyekiti
wa mkoa wa Lindi, ndugu Ally Chitanda, chadema hakujibu hoja zake wakamkana
·
Mzee
EDWIN MTEI alipotoa kauli kwamba TUME YA MABADILIKO YA KATIBA ni ya KIDINI na
kwamba KIKWETE ameteua WAISLAM WENGI kuliko wakristo, MBOWE AKAMKANA
·
JOSHUA
NASSARY alopotoa kauli kwamba mikoa ya KASKAZINI itajitenga na kuanzisha nchi
yao ya JAMUHURI YA KASKAZINI, Mbowe akamkana.
·
Hata
MBOWE mwenyewe alipotangaza Hadharani kwamba amerudisha gari la kiongozi wa
UPINZANI BUNGENI na kwamba halitaki tena, AKAJIKANA na AKAENDELEA KULITUMIA
MPAKA LEO
·
Hata
MNYIKA na LISSU na wabunge wengine walipotangaza kutokuchukua POSHO BUNGENI,
WALIJIKANA NA WANAENDELEA KUCHUKUA MPAKA SASA
·
Hata
MBOWE na SLAA walipotangaza kwamba CUF
ni CCM B na MBATIA ni kibaraka wa CCM WAKAJIKANA na leo Wamejiingiza humo humo
na kuungana nao
Hivyo tunawataka wawe na hulka za
kujibu hoja na sio kukimbilia kuwakana watu ambao ni wanachama halali.
Sasa kama kilan atakayekosoa
anakanwa, nani atabaki?, nani mwanachama halali, MBOWE na SLAA TU ama?.
Tamko hili limesomwa leo 25.6.2014
na;-
JORUM
ABDALLAH MBOGO
………………………………………..
MWANACHAMA
WA CHADEMA
MWENYEKITI
WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE
WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE
WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Tunaambatanisha na nakala za Barua za
kwa Msajiri na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu.
MDHIBITI
NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
MTAA WA
SAMORA NA OHIO
S.L.P
9080
DAR ES
SALAAM
DAR ES
SALAAM.
Ndugu.
YAH: MAOMBI YA
TAARIFA YA UKAGUZI WA CHADEMA.
Husika
na somo hapo juu.
Mimi ni
mwanachama na kiongozi wa ngazi ya wilaya wa Chama cha Demokrasia na maendeleo
(CHADEMA) ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la chama
Kwa
kipindi kirefu ndani ya chama chetu tumekuwa tukilalamikia matumizi mabaya ya
pesa hasa za ruzuku, pesa ambazo msingi wake ni kodi za wananchi na hivyo kuwa
ni pesa za umma. Hii inatokana na ukweli kwamba mpaka sasa chama kimepokea
jumla ya BILION 10.038 kama ruzuku
kutoka serikali kuu, kwa kipindi cha miezi 42 kutokea uchaguzi mkuu wa mwaka
2010
Tumejitahidi
sana kudai taarifa sahihi za matumizi ya pesa hizo bila mafanikio.
Kwa
kuwa tunatambua kwamba ni hivi karibuni tu, ofisi yako imemaliza kufanya UKAGUZI MAALUM WA MAHESABU KWA VYAMA VYA SIASA kikiwemo na CHADEMA, na kwamba taarifa yake mmeshaiwasilisha
Bungeni.
Kutokana
na ukweli kwamba wengi wetu sisi sio wabunge na hatuna uwezo wa kuipata hiyo
Taarifa ambayo ni muhimu sana.
Na kwa
kuzingatia kwamba sisi ndio wenye chama na sisi ndio walipa kodi zinazoipatia
chama Ruzuku. Ni wajibu wetu kusimamia matumizi yake.
Hivyo
basi, kwa niaba ya viongozi na wanachama wenzangu wasiopungua 82, tunaiomba
ofisi yako itusaidie yafuatayo
1. ITUPATIE NAKALA YA TAARIFA ILIYOKAGULIWA
2. IITOE NAKALA HIYO KWA UMMA ILI UMMA UJUE NAMNA KODI ZAO
ZINAVYOTUMIWA
Tunatumaini
kwamba Ombi letu litashuhulikiwa kwa uzito na umuhimu wa kipekee
Tunatanguliza
shukrani zetu za dhati.
Wako
katika ujenzi wa Taifa
……………………………………………………
JORUM
ABDALLAH MBOGO
MWANACHAMA
WA CHADEMA
MWENYEKITI
WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE
WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE
WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Nakala
:- Vyombo vya habari
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
S.L.P 63010
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Ndugu,
YAH: MAOMBI YA UFAFANUZI WA KIKATIBA JUU YA UVUNJIFU WA KATIBA NA YA CHAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI
Mheshimwa
Msajiri, Somo hapo juu la husika.
Mimi ni mwanachama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
Kwa niaba ya wanachama wenzangu,
tunaleta kwako malalamiko ya uvunjifu wa
katiba ya chama Yanayotokana na
matamko yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kitaifa juu ya kuungana na UKAWA
yenye tafsiri kwamba wataachiana majimbo ya kugombea ili waweze kuingia
madarakani na kuunda serikali ya pamoja.
kama hivyo ndivyo wanakiuka
SURA YA TISA. IBARA YA 9.3.1 ya KATIBA
YA CHADEMA inayosema ‘’chama
kinaweza kuunda mseto na chama au vyama vingine vyenye madhumuni na malengo
yanayofannaili kuimarisha iwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au wa serikali moja
ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja’’
Kwa kuwa viongozi wa CHADEMA na CUF na
NCCR wameungana na kuunda chama kingine cha UKAWA kwa mujibu wa SURA YA TISA
ibara ya 9.3.3 ‘’chama kinaweza kuungana na chama ama vyama vingine kuunda chama
kipya’’ hivyo wamevunja SURA TISA, Ibara ya 9.3.4 inayosema ‘’Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1, na 9.3.3
utafanywa na mkutano mkuu wa Taifa na kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza KUU’’.
Na hivyo sisi kama chama hatujakaa BARAZA
KUU ili kupitisha AGENDA za huo mkutano mkuu na wala MKUTANO mkuu haujaitishwa
kujadili maamuzi hayo yaliyofikiwa na viongozi wetu.
Mheshimiwa Msajiri, Tunafahamu kwamba
KANUNI za chama SURA YA TISA kuanzia ibara ya 9.0 Mpaka ibara ya 9.7 zinatoa
uhuru wa chama kuungana na kufanya ushirika na vyama vingine kwa kadri
itakavyoona inafaa.
Ila kanuni hizi zinaweka mkanganyiko wa
kitafsiri, na hivyo zinazuiwa na kuuliwa nguvu na Ibara ya 9.2.3
ya KATIBA YA CHAMA Inayosema ‘’kukitokea
migongano kati ya kipengele cha katiba na kile cha kanuni, kipengele cha katiba
kitatawala’’. Hivyo kanuni zinazotoa uhuru huo haziwezi
kutumika hapa.
Mheshimiwa msajiri, kwa kuwa wewe ndio
mlezi na msimamizi wa vyama vyote vya siasa, na kwa kuwa hakuna chama cha siasa
kilicho juu ya katiba yake, hivyo tunakuomba uingilie kati mgogoro huu wa
uvunjifu wa katiba unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa chama.
Tunakuomba pia uuagize uongozi wa
kitaifa uitishe haraka kikao cha baraza kuu, kwani tumeshapitisha miezi mi nne
sasa ya kisheria ambayo baraza kuu lilipaswa kukaliwa, mara ya mwisho tulikaa
kikao cha baraza kuu mwezi febryary mwaka 2013, hivyo tulitakiwa tena tukae
baraza kuu mwezi February mwaka huu. Hatujaitwa, wala hatujapewa sababu yoyote
yenye mantiki.
Vile vile tunakuomba uwaagize viongozi
wa chama waitishe chaguzi halali za zhama na waache kuchomeka watu wao
wanaowataka kwa hila, kwa mujibu wa ratiba tulizozipitisha uchaguzi ulupiswa
kuwa umeshafanyika kufikia December 2013, na baadae june 2014, lakini mpaka
tunavyokuandikia leo, hakuna lililofanyika.
Tunakutakia kila la heri katika
kutusaidia ufafanuzi huu.
Tunatanguliza shukrani za dhati na
tukiamini swala letu litafanyiwa linavyostahili.
Wako katika ujenzi wa Taifa.
JORUM
ABDALLAH MBOGO
………………………………………..
MWANACHAMA
WA CHADEMA
MWENYEKITI
WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE
WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE
WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
No comments:
Post a Comment