Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkunguni, Stendi ya
Mabasi, katika Kisiwa cha Mafia, leo, Septemba 16, 2014, ikiwa ni
mwendelezo wa ziara yake katika mkoawa Pwani. Kinana amewataka viongozi
wa CCM kisiwani humo, kuachana na maswala ya kufitiana kwa ajili ya
kusaka uongozi badala yake wajikite zaidi ya maswalaya maendeleo ya
wananchi kwa sababu kufanya hivyo ndiyo kutaimarisha chama na kukifanya
kipendwe zaidi na wananchi.
Mamia ya wananchi wa Mafia wakiwa kwenye mkutano huo wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafia kwenye uwanja wa Mkunguni stendi ya Mabasi mjini Mafia.
Naibu
Waziri Nishati Charles Kitwanga akihutubia wakazi wa Mafia ambapo
aliwaambia Mafia ndio wilaya pekee itakayopata Umeme kwa asilimia mia
moja.
No comments:
Post a Comment