Katibu
Mkuu wa CCM, akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari
kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda Nyamisati wilayani Rufiji, baada ya
kumaliza ziara yake katika wilaya ya Kisiwa hicho, akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani, kukagua utekelezaji wa ilani
ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya
kuzitatua katika mkoahuo. Boti hiyo ambayo pia hutumiwa na wananchi
kusafiria kati ya kisiwa hicho cha Mafia na Nyamisati Kinana amesafiri
nayo kwa saa nne tangu saa sita mchana hadi saa 11 jioni.
Katibu Mkuu wa CCM akipanda boti hiyo kwa ukakamavu
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye boti hiyo. Kushoto ni Mkuu
wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, ambaye aliwasili wilayani Mafia kwa
ndege lakini akalazimika kusafiri na Kinana kwa boti hiyo kurejea
Nyamisati. Watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani
Mwinshehe Mlao.
Katibu
wa NEC, Itikadina Uenezi, Nape Nnauye (watatu kushoto), akiwa kwenye
boti na abiria wengine waliosafiri pamoja na Kinana kutoka Mafia hadi
Nyamisati.
Baadhi
ya maofisa wa CCM na Waandishi wa habari wakiwa kwenye boti hiyo wakati
wakisafiri na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Umma wa Makao Makuu ya CCM, Daniel Chongolo (watatu
kushoto) akiwa na abiria wenzake katika boti hiyo kutoka Mafia hadi
Nyamisati.
Abiria
wengine wakiwa katika boti hiyo kutoka Mafia kwenda Nyamisati.Kushoto ni Mwandishi wa Clouds TV/Radio Salum Mwinyimkuu.
Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Mama Salma Kikwete ya Wama iliyopo wilayani Rufiji, baada ya kutoka
Mafia. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Suma Mesa. Kinana amempongeza Mama
Salma kwa uamuzi wake wa kuanzisha shule hiyo ambayo ni maalum kwa
ajili ya kutoa elimu kwa watoto yatima kutokamikoa mbalimbali nchini.
Watoto wa shule hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Kinana.
Kinana
akiondoka kwenye shule hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani
Mwinshehe Mlao na watatu kushoto ni Mwandishi wa habari wa gazeti la
Jamboleo, Saidi Mwinshehe na kulia ni Chongolo. Kinana anatarajiwa
kuendele na ziara yake katika mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment