KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, September 17, 2014

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA YATOA TAARIFA KUHUSU MWITIKIO DHIDI YA UKIMWI KWENYE BARABARA ZA KIMATAIFA NCHINI KUPITIA VITUO VYA MAARIFA.

 Mratibu wa Mpango Maalumu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Renatus Kihongo.
 Ofisa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TACAIDS, Nadhifa Omar. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Ofisa Habari wa TACAIDS, Godlease Malisa.
 Mratibu wa Mpango Maalumu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Renatus Kihongo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu mwitikio dhidi ya ukimwi kwenye barabara za kimataifa nchini kupitia vituo vya maarifa. Kulia ni Ofisa Habari wa TACAIDS, Godlease Malisa na Ofisa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TACAIDS, Nadhifa Omar.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale

TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeandaa mpango wa kujenga  vituo vya maarifa kwa ajili ya huduma ya utoaji elimu ya kuhusu ukimwi kwa madereva wa masafa marefu.


Akizungumza  Dar es Salaam leo, Mratibu wa Mpango Maalum,  Renatus Kihongo, alisema madereva na wasafirishaji wa mzigo inayopelekwa masafa marefu hutumia muda mrefu kukaa mbali na familia zao hivyo kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Hali ya maambukizi katika nchi kwa tafiti zilizofanyika mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Manyara imekua ikiongoza kwa maambukizi.

"Hali hii inasababisha maingiliano ya kingono baina ya wasafirishaji na wenyeji wa eneo husika na pia makundi ya wauza ngono ili kujipatia kipato,"alisema.

Alisema hadi sasa vituo ambvyo vimekamilika ni 14 katika maeneo ya barabara kuu ambapo malori hayo yanalala 

Vituo hivyo ni Kagongwa Kahama,Kibaingwa Kongwa,Mdaula Bagamoyo Uvinza na Kazuramimba ,Kasula na Benacco.

Aidha vituo vingine ni bandari ya Temeke Dar es Salaam,Chalinze Makambako Tunduma,Mbozi -Mbeya Ilemela-Mwanza.

Aliongeza kuwa ujenzi wa vituo hivyo utaendelea kuongezeka hadi kufikia 21 lengo likiwa kutokomeza ukimwi katika nchi zote zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara na nchini.

No comments: