Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam.Wengine Naibu waziri Wizara ya Afya na Utalii wa Australia Magharibi Dk,Kim Hames (wa pili kushoto) Balozi wa Australia nchini John Feakes na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba.
Naibu waziri Wizara ya Afya na Utalii wa Australia Magharibi Dk,Kim Hames.
Wageni waliohudhulia sherehe ya kusaini makubaliano.
Wageni.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi (kulia) na Naibu waziri Wizara ya Afya na Utalii wa Australia Magharibi Dk,Kim Hames (kushoto) wakitia saini makubaliano wakishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba(kulia) pamoja na Balozi wa Australia nchini John Feakes.
Wakipongezana baada ya kusaini.
Wakiwa katika picha ya pamoja viongozi walioshuudiwa kutia saini makubaliano hayo.
Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepata msaada kutoka Serikali ya Australia
kupitia Idara ya Biashara na Mambo ya Nje (DFAT) wa kutengeneza mfumo wa namna ambavyo
VETA itakuwa ikishirikiana na viwanda pia waajiri mbalimbali katika kutoa
mafunzo ya ufundi stadi. Mfumo huo utakuwa ndio mwongozo wa kuainisha utaratibu
wa mafunzo ya ufundi na viwanda au sekta mbalimbali za uchumi mfano sekta ya
madini, gesi, utalii n.k.
Mfumo huu
utatengenezwa na wataalamu kutoka Australia na Serikali ya Australia imekubali
kutoa fedha kiasi cha TSh. 330 milioni kwa ajili ya kazi hiyo.
Manufaa
ya mfumo huo kwa VETA itakuwa:-
1)
Kuimarisha mashirikiano na viwanda au
waajiri mbalimbali ili kulenga kutoa mafunzo ambayo yanaendana na mahitaji ya
soko la ajira.
2)
Utaboresha viwango vya mafunzo
yanatolewa na viwanda.
3)
Utapunguza mzigo unaobebwa na Serikali
katika kugharamia mafunzo ya ufundi stadi kwa vile viwanda vitakuwa na fursa ya
kuchangia gharama za mafunzo kwa njia ya vifaa au kutoa wataalamu wa
kufundisha.
4)
Pia walimu wa VETA watakuwa
wanajengewa uwezo maana mfumo utawawezesha kufanya mazoezi ya vitendo
(practical training) viwandani mara kwa mara ili kunoa ujuzi wao.
5)
Mashirikiano
haya yatafungua fursa nyingi za ushirikiano na Taasisi mbalimbali za mafunzo ya
ufundi stadi nchini Australia hasa tukizingatia kuwa Australia ni miongoni mwa
nchi zinazoongoza kwa mafunzo ya ufundi stadi.
Makubaliano
ya msaada huo yametiwa saidni leo 27 Mei, 2015 kati ya VETA na Idara ya Biashara na Mambo ya Nje ya Australia katika
Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam
Balozi wa
Australia Mheshimiwa John Feaks na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah
Moshi walisaini makubaliano hayo huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri Mkuu wa
Jimbo la Australia ya Magharibi, Bw. Kim Hames na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Tanzania), Bi. Consolata Mgimba.
Balozi
wa Australia alisema kuwa, Serikali yake imeamua kuisaidia VETA ili kuimarisha
taasisi za elimu na mafunzo ya ufundi na hivyo kuwa na uwezo wa kutoa wahitimu
wenye ujuzi wa kutenda kazi katika eneo la gesi, mafuta na madini.
Alisema
kuwa msaada huo utalenga zaidi katika kugharimia ushauri wa kitaalam kwenye
kuandaa mitaala na kujengea uwezo walimu wa mafunzo ya ufundi stadi.
Australia
imefurahi sana kuisaidia VETA katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa Watanzania
wako katika nafasi nzuri za kutumia na kunufaika na fursa za uwekezaji katika
sekta ya madini, gesi na mafuta nchini mwao,” alisema.
Upatikanaji
wa wafanyakazi wenye ujuzi wa aina mbalimbali unayapa makampuni makubwa ya
uwekezaji fursa ya kuajiri wafanyakazi kutoka ndani ya nchi na hivyo
kuwanufaisha wao wenye makampuni na jamii ya ndani, kukuza uchumi wa nchi,
hususani kwa kuwapatia wananchi ajira na vipato,” alisema Feakes.
“Tukiwa
na uwezo na uzoefu mkubwa katika mafunzo ya ufundi stadi kwenye eneo la mafuta,
gesi na madini, tuko radhi kuisaidia Tanzania kunufaika na sekta hiyo,”
aliongeza.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Consolata Mgimba
aliishukuru serikali ya Australia na kusema msaada huo utachangia kwa kiasi
kikubwa katika kuwawezesha vijana wa Kitanzania kuajirika, utaongeza tija
mahali pa kazi na kuchochea ukuaji wa viwanda.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA alisema kuwa pamoja na kupata msaada wa
kifedha, VETA inatarajia kunufaika kwa kiasi kikubwa na utaalam na uzoefu
kutoka Australia kwa kuwa nchi hiyo ina uzoefu na ujuzi mkubwa kuhusu ushirikiano
kati ya taasisi za elimu na mafunzo ya ufundi
kwa upande mmoja na viwanda kwa upande mwingine.
Alisema
kuwa ushirikiano huo utasaidia kuboresha mfumo wa elimu na mafunzo ya ufundi
stadi nchini Tanzania.
“Kuwa na mfumo
wenye ushirikiano kati ya viwanda na taasisi za mafunzo ya ufundi stadi ni
muhimu sana. Ni kupitia mfumo huo ambapo kunakuwa na uhakika wa kutoa
rasilimali watu yenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya waajiri, inahakikisha
ubora na inawahakikishia wahitimu kuajirika”, Alisema Mhandisi Moshi.
Mfumo huo pia
unaweza kuisaidia serikali kupata ahueni ya kugharimia elimu na mafunzo ya
ufundi stadi kwa kuwa wenye viwanda wanaweza kuchangia katika utoaji wa elimu
na mafunzo ya ufundi stadi.
Kwa
mawasiliano zaidi
Sitta Peter
Meneja
Uhusiano
Barua
pepe: speter@veta.go.tz
Simu:
0767920019/0652226688
No comments:
Post a Comment