Michuano ya UMISETA
ngazi ya taifa imemalizika leo asubuhi huko jijini Mwanza kwa mchezo wa fainali
kati ya Dar es salaam dhidi ya Nyanda za juu Kusini wavulana, huku fainali
nyingine kwa upande wa wasichana ikipigwa jana kati ya Dar es salaam dhidi ya
Kanda ya Mashariki.
Katika fainali
ya jana wasichana, Dar es salaam wametawazwa kuwa mabingwa baada ya kuwatandika bila huruma Kanda ya Mashariki
kwa mabao 7-1,kwenye mchezo uliokuwa na msisimko mkubwa kwa Dar es salaam kuonesha
uwezo mkubwa wa kusakata kandanda.
Dar es
salaama ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuisukumiza nje Kanda ya
Ziwa mabao 4-1,huku Kanda ya Mashariki ikifanikiwa kutinga katika hatua ya
fainali baada ya kuifunga Kanda ya Kaskazini kwa mabao 3-1.
Kwa upande
wa fainali ya wavulana leo asubuhi,Nyanda za Juu Kusini wametawazwa mabingwa
baada ya kuifunga Dar es salaam bao 1-0,bao ambalo ni la kujifungwa baada ya
mabeki wa Dar kujichanganya katika harakati za kuokoa hatari langoni mwao.
Nyanda za
Juu Kusini walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Kanda ya
Ziwa kwa mabao 3-0,huku Dar es salaam wakitinga hatua hiyo baada ya kuifunga
Zanzibar ambao ndio walikuwa mabingwa wa tetezi kwa mabao 4-3.
Chama cha
soka mkoa wa Dar es salaam DRFA chini ya mwenyekiti wake Almas Kasongo,kimeelezwa
kufurahishwa kwake na mafanikio yaliyooneshwa na vikosi hivyo vilivyo katika
himaya yake (Dar es salaam),na kuviomba vilabu vya ligi mbalimbali kujitokeza
kuangalia mashindano ya vijana ili kupata wachezaji wa baadaye kwenye vilabu
vyao.
LIGI YA WANAWAKE
DAR YASUBIRI RATIBA YA TWIGA STARZ.
Ligi ya
wanawake mkoa wa Dar es salaam iliyomaliza mzunguko wake wa kwanza,ipo katika
maandalizi ya kuanza mzunguko wa pili na wa mwisho kumpata bingwa wa ligi hiyo.
Kamati ya
mashindano ya DRFA,imesema kinachosubiriwa kwa sasa ni ratiba ya benchi la
ufundi la timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars,ambao wapo kambini kujiandaa na
michuano ya afrika (All African Games) huko Congo Brazavile,mwezi Septemba
mwaka huu.
Mpaka sasa
kikosi cha Mburahati Queens ndicho kinachoshikilia usukuni wa ligi kwa kuwa na
pointi 18,nafasi ya pili inashikiliwa na Evergreen Queens wenye pointi 12,sawa
na JKT Queens wenye pointi 12 katika nafasi ya tatu wakitofautiana magoli.
No comments:
Post a Comment