Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo
ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
mholanzi Mart Nooij.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika
hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele ya vyombo
ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa
kuanza kazi.
“Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania
tunasafari ndefu katika mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza
katika soka la vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa”
alisema Malinzi.
Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la
vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira katika
umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi
bora.
Nchi za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya
Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya
nchi wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la
vijana
TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13,
U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki
ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania
kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016.
Kikosi cha U15
kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za
Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani
mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza
michezo ya kirafiki.
Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa
Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru watanzania
wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti
waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.
Nooij
alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote
alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho
wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka
Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.
Wakati huo
huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha
mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni
kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi
cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania
kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao
wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A
ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani
wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa wamekizi.
Kocha
Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho)
alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua
benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa
mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao
wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha Kamati ya utendaji ya TFF
Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la
uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na
timu ya Taifa.
U15 YAINGIA KAMBINI
Timu ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia kambini jana
na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo wa
kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya jumapili.
Kikosi
hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza
mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na
kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.
U15 ni mpango
wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka
fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar,
ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati
michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
NB: Kesho
siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na msaidizi
wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30 asubuhi
katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.
Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment