Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu
kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe
11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier
League msimu wa 2014/2015.
Hafla ya
utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte
(Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa
wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.
Mgeni
rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu
washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo.
Vodacom
watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili,
mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa
zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :
1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
- Mohamed Hussein (Simba SC)
- Mrisho Ngasa (Young Africans)
- Saimon Msuva (Young Africans)
2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
- Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
- Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
- Shaban Hassan (Coastal union)
3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
- Goran Kopunovic (Simba SC)
- Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
- Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)
4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
- Israel Mjuni Nkongo
- Jonesia Rukyaa
- Samwel Mpenzu
5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
- Mgambo JKT
- Mtibwa Sugar
- Simba SC
MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI
Wakati
huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi
wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.
Kwa
kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu
sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment