Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu.
Philomena Marijani
Advocacy and Communications Manager
WAMA Foundation
P.O. Box 10641, Luthuli Street
Dar es Salaam
Office Tel: +255 22 2126516
Office Fax: +255 22 2121916
Mobile: 0754 439 183
www.wamafoundation.or.tz
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) inatangaza nafasi za kidato cha kwanza kwa wasichana katika Shule zake mbili
za Sekondari:
(1) Shule ya Sekondari WAMA - Nakayama
iliyopo Kijiji cha Nyamisati Wilaya ya Rufiji , Mkoa wa Pwani:
(2) Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf iliyopo Mitwero
katika Manispaa ya Lindi
WAMA ni Taasisi isiyo ya kiserikali
iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia maendeleo ya wanawake na
watoto. WAMA inaendesha shule hizi maalum kwa ajili ya watoto yatima na
wanaotoka katika mazingira magumu. Hata hivyo, WAMA inatoa fursa chache kwa
wanafunzi wengine ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia ili kuongeza uwezo wa
kusaidia watoto wengi zaidi.
Tunafurahi kutoa fursa hii kwa wasichana
ambao wataweza kulipia ada kwa kidato cha kwanza katika shule zote mbili kwa
mwaka 2016.
Fomu za kujiunga zinapatikana katika
ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam zilizopo Kawe
karibu na Hoteli ya Picolo Beach au katika Tovuti ya Taasisi: www.wamafoundation.or.tz
Kwa wakazi wa Lindi fomu
zinapatikana katika Ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) tawi la
Lindi zilizopo katika makutano ya
Barabara ya Karume na Amani , Kiwanja no.11 kitalu B karibu na Ofisi za Magereza za Mkoa wa Lindi
Kwa Dar es Salaam mtihani wa
kujiunga na shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika Alhamisi Novemba
12, 2015 katika Shule ya Sekondari Jangwani.
Kwa Lindi mtihani wa kujiunga na
shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika Alhamisi Novemba 19 , 2015 katika
Chuo cha VETA Lindi.
Mwanafunzi anatakiwa arudishe fomu
pamoja na risiti ya malipo katika ofisi za Taasisi ya WAMA au kwa kutumia barua
pepe: info@wamafoundation.or.tz, mbugunimwajuma@gmail.com na alimindria66@yahoo.com.
Mwisho wa kurudisha fomu ni Jumatano
tarehe 11 Novemba, 2015.
Shule zetu zina mazingira na huduma
zote muhimu zinazowawezesha wanafunzi kufaulu vizuri yakiwemo mabweni ya
kisasa, maabara za kisasa, maabara za computer, maktaba zenye vitabu vya
kutosha na walimu wazuri na wakutosha.
Kwa
Mawasiliano zaidi:
Piga Namba: 0685-651449, 0789-000341, 0754-439183,
Barua pepe: info@wamafoundation.or.tz
Tovuti: www.wamafoundation.or.tz
No comments:
Post a Comment