Na Mwandishi Maalum – Maelezo
Vyombo vya
habari nchini vimepongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kutoa taarifa kwa
wananchi wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa 10 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa
leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel wakati akiongea na viongozi wa menejimenti ya wizara na taasisi zake
kwenye kikao cha kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Prof. Gabriel alisema kipindi
cha uchaguzi vyombo vya habari vilifaya kazi kubwa ya kuwahabarisha wananchi
habari za uchaguzi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yao na hivyo kuwawezesha wananchi
kujua mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea hapa nchini.
Katibu Mkuu huyo ambaye
hicho kilikuwa ni kikao chake cha kwanza tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa
wizara hiyo mwishoni mwa mwezi wa kumi aliahidi kuwatumikia na kuwaheshimu wafanyakazi
wa wizara yake huku akisimamia majukumu ya kazi kwa kufauata kanuni, taratibu
na sheria za utumishi wa Umma.
“Hiki ni kikao chetu cha
kujipanga kwa ajili ya kazi, ni vyema tukajipanga huku tukijuwa matarajio ya Mhe. Rais kwetu ni yapi, wananchi tunaowatumikia
wanategemea kupata nini kutoka kwetu na mimi
kama Katibu Mkuu natarajia kupata nini kutoka kwenu”, Prof. Gabriel alisema.
Akimkaribisha Katibu Mkuu
huyo kuongea na viongozi hao Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu
Titus Mkapa alisema kikao hicho ni maalum kwa ajili ya wizara kujadili
utekelezaji wa mipango ya wizara kwa kasi.
Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti viongozi hao waliiomba
Serikali iangalie upya bajeti ya wizara hiyo ambayo ni ndogo ili iweze
kuongezwa na kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufaisi zaidi.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TasuBa) Michael
Kadinde alisema chuo hicho kimekuwa kikizalisha ajira kwa wanafunzi wanaosoma
hapo mara baada ya kumaliza masomo yao lakini wanafunzi wengi wanakabiliwa na
changamoto ya kutokuwa na ada.
“Kuna baadhi ya wanafunzi
wanajiunga na chuo hiki wakiwa na elimu ya darasa la saba, na hivi sasa
Serikali itaanza kutoa elimu bure kwa wanafunzi kwa darasa la kwanza hadi
kidato cha nne”.
“Ninaiomba Serikali iweze
kuwaangalia wanafunzi hawa wa darasa la saba ambao wanasoma chuoni kwetu ili
nao waweze kupata elimu bure sawa na wanafunzi wa Sekondari”, alisisitiza
Kadinde.
Kikao hicho kimeitishwa
kufuatia kikao cha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Makatibu wakuu,
manaibu makatibu wakuu na watendaji wakuu wa Serikali kilichofayika mwishoni mwa wiki ambapo alieleza
matarajio yake na matarajio ya wananchi katika uongozi wake. Hivyo aliagiza
kila sekta ikae na kujipanga kufanya kazi ili kukidhi matarajio ya wananchi.
No comments:
Post a Comment