Na Jaffar Haniu Ikulu
Ndege mpya ya PILI
iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya
kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada
ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya
Bombadier Dash - 8 Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:50 Mchana na kisha
kupatiwa heshima maalum kwa kumwagiwa maji na magari ya zimamoto (Water Salute).
Akizungumza baada
ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema baada
ya kuwasili kwa ndege zote mbili uzinduzi rasmi utafanyika kesho Jumatano
kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt.Chamriho amewataka
wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi
amesema ATCL imejipanga kuingia katika soko la ushindani na kuwaahidi
watanzania huduma nzuri na bora katika kuhakikisha wanasafiri kupitia sekta
hiyo ya anga,kwa usalama na bei nafuu.
Ndege hii ya pili
imewasili ikiwa ni wiki moja baada ya ndege
ya kwanza iliyowasili tarehe 20 Sept 2016.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
No comments:
Post a Comment