KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, March 10, 2018

UFUNGUZI WA MASHINDANO YA SPORTS XTRA NDONDO CUP 2018.



Shaffih Dauda-M/kiti kamati ya Ndondo Cup
UTANGULIZA
Karibuni sana kwenye mkutano maalumu wa ufunguzi wa mashindano ya Sports xtra Ndondo cup 2018, ikiwa ni msimu wake wa tano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014.
Kama mnavyofahamu Ndondo CUP inahusisha timu za mitaani tunakotoka na lengo lake mama ni kuwapa nafasi vijana wenye vipaji vya kucheza mpira kuweza kuonekana na wadau wengine kama ambavyo Clouds Media tunavyosema tunakufungulia dunia kuwa unachotaka.
Sasa kwa misimu yote minne tumekua na mabadiliko katika kila msimu ya uboreshaji na kuifanya Ndondo CUP kuwa maisha halisi ya mtanzania katika kila angle mbali tu na kuchezwa mpira bali tutaangali vyakula vyetu, music wetu, na tabia zetu kwa ujumla,  tunasema (life style) ya uswahilini kwetu.
Msimu wa tano tunataka kuwekeza zaidi katika mtazamo huo, mpira wa miguu kwa maana ndani ya uwanja iwe asilimia 40 tu, lakini asilimia 60 zinazosalia iwe ni mambo mengine yaliyo nje ya uwanja kama nilivyoeleza hapo awali.
Ndondo cup iwe ni mtoko halisi unapokuja katika viwanja vyetu tunavyovitumia basi uwe na uwezo wa kupata mahitaji muhimu kama chakula chetu cha kindondo mfano tu wali maharage, miguu ya kuku, mihogo, uji wa mchele, pweza kidogo na mahitaji mengine tunayoyapata hata tukiwa maskani mwetu.
Burudani ya music, show za wasanii na ulinzi wa kutosha ni vitu ambavyo tumekua tukiishi navyo tangu tulipoanza mwaka wa kwanza na yote mtakua mashahidi wa hili..
Ukuaji wa mashindano haya nao hauko nyuma tulianza mwaka jana kwa kuongeza mikoa miwili ya Mwanza na Mbeya na hivyo hivyo mwaka huu tutaendelea kuwa na mikoa mingine miwili nje ya Dar es salaam.
Kwa kushirikiana na vyama vya soka vya mikoa husika naamini tutafanikisha azma yetu ya mpira kuchezwa na vijana wenye vipaji kuonekana.
Kwa maelezo hayo mafupi leo tunazindua msimu mpya wa ndondo cup 2018 ukiwa na kauli mbiu (slogan) "WASHTUE WANAAAA" kama ilivyokua utaratibu wetu.
Na mwaka huu Ndondo Cup itafanyika mkoa wa Mwanza kama ilivyokua mwaka jana lakini pia tumeuongeza mkoa wa Ruvuma ambao unachukua nafasi ya Mbeya .

KUHUSU USAJILI WA TIMU
Baada tu ya kumalizika press hii zoezi la usajili wa timu kwa mkoa wa Dar es salaam utaanza rasmi kupitia usimamizi wa chama cha soka mkoa huo (DRFA) kupitia kamati yake ya mashindano kwa ada ya ushiriki kiasi cha shilingi laki tatu (300,000)/= ambazo zitalipwa kupitia account  ya DRFA.
Kwa wale wa mikoani tutawajulisha zoezi la usajili wa timu utafanyika kuanzia lini, lakini ada ya ushiriki itakua laki tatu (300,000) kwa mikoa yote.
ZAWADI
Kila mwaka tumekua na maboresho katika zawadi inawezekana haikua ya fedha lakini kuna upande mwingine kuna kitu kiliongezeka mfano mwaka jana tuliongeza tuzo maalum ambazo sisi tunaamin ni muhimu sana kwa mchezaji.
Mwaka huu hakutakua na ongezeko la fedha kwenye zawadi za mwisho itabaki kama ilivyokua kwa bingwa milion kumi, mshindi wa pili milion tano na mshindi wa tatu milion tatu lakini mwaka huu tumeongeza hadi mshindi wa nne atapata milion moja.
Lakini tulichofanya ni kuboresha kwa kuzipa fedha ya maandalizi timu ambazo zitafanikiwa kuingia hatua ya mtoano kuanzia 16 bora ambapo timu zote zitakazo ingia hatua hiyo tutazipa laki tano kila moja kwa maandalizi.
Timu 8 zitakazoingia robo fainali tutazipa milion moja moja kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao hali kadhalika timu nne zitakazoingia nusu fainali nazo zitapewa kiasi cha shilingi milion moja na nusu kwa kila mmoja kwa ajili ya maandalizi.
Na zile timu mbili zitakazoingia fainal zitapewa milion mbili za maandalizi.
Ikipiga hesabu vizuri utagundua timu itakayo kuwa bingwa itakua imekusanya milion 15 lakini hawa wengine nao watakua wamepata fedha.
Mbali na zawadi ya fedha mwaka huu tutazipa timu usafiri kwa ajili ya wachezaji kuanzia hatua ya 16 bora kuwapeleka uwanjani na kuwarudisha.
Lakini pia tunafahamu changamoto zinazowakabili timu wakati wa maandalizi na kama nilivyosema toka mwanzo ndondo inaenda hadi kwenye utamaduni wa chakula hivyo tumu zinazoingia hatua ya 116 bora nazo tutazipa chakula cha mchana kwa wachezaji na viongozi wasiozidi 30.
Tutaendelea kuwa na zawadi za mtu mmoja mmoja kwa maana ya mfungaji bora, mchezaji bora, kipa bora, kocha bora, mchezaji chipukizi n.k
Kikundi bora cha ushangiliaji zawadi yake itaendelea kuwa milion moja lakini tutakua na zawadi ya shabiki mmoja mmoja ambazo zitakua kwa shabiki watano maana tumegundua kuna mashabiki wanafanya vizuri lakini sio kundi na kukosa nafasi ya kupata zawadi.
Utaratibu huu wa zawadi ni kwa mkoa wa Dar es salaam pekee
ZAWADI MWANZA
Bingwa atapata milion tano kutoka tatu za mwaka jana, mshindi wa pili milion tatu na mshindi wa tatu milion mbili. Pia zawadi za mshindi mmoja mmoja itabaki kama ilivyokua shilingi laki tano.
Bila kusahau kikundi bora cha ushangiliaji ni milion moja

ZAWADI RUVUMA
Bingwa atapata milion tatu, mshindi wa pili milion mbili na mshindi wa tatu milion moja, mshindi mmoja mmoja watapata zawadi ya fedha shilingi laki tano.
Bila kusahau kikundi bora cha ushangiliaji ni milion moja

WADHAMINI
Mwaka jana kama tunakumbuka vizuri hatukua na mdhamini mkuu, lakini mwaka huu tupo na mCheza Tanzania ambao ni kampuni ya mchezo wa kubashiri matokeo, tutakua nao pia BEKO ambao ni watengenezaji wa vifaa vya kieletroniki vya majumbani, Macron watengenezaji na wasambazaji wa vifaa vya michezo kutoka Italy, ambao watatoa vifaa kwa timu 32 shiriki hatua ya makundi, lakini pia watatuma mascout katika hatua ya 16 bora kwa ajili ya kuwapeleka katika klabu ya Bologna ya italia ambayo ipo chini yao, bila kuwasahau Azam Tv ambao tumekua nao tangu mwaka wa kwanza wa mashindano.
Pamoja na kuwepo kwa hawa bado milango ipo wazi kwa wadau wengine kwa sababu bila nguvu ya wadhamini ki ukweli changamoto ni nyingi.
UTARATIBU WA WAANDISHI WA HABARI (ACCREDITATION)
Kwa waandishi wa habari tutaendelea na utaratibu wa kujisajili kwa njia ya mtandao ili kupata access ya kuripoti au kuingilia uwanjani.
Na mwaka huu tutajitahid kuboresha zaidi mazingira ya wana habari ili kuwapa nafasi ya kufanya kazi zao kwa ufanisi.
RATIBA YA MASHINDANO

RATIBA YA MATUKIO YA SPORTS XTRA NDONDO CUP  2018
NO.
TAREHE
TUKIO
ENEO
1.
9  March 2018
Press conference-Ufunguzi msimu
Kuanza kwa Usajili  wa timu shiriki
Dar es salaam (escape one)
Ruvuma
Mwanza
2.
6 April - 6 May 2018
Hatua ya awali
Dar es Salaam
Viwanja....
v  Kinesi
v  Mabatini tandika
v  Benjamini mkapa
v  Ukombozi
v  Airwing ukonga
v  Bandari
3.
25 May  2018
v  Hafla ya upangaji makundi 32 bora.
v  Semina kwa viongozi wa timu shiriki.
v  Ugawaji wa vifaa kwa timu na waamuzi.

Dar es Salaam (escape 1)
4.
1 June - 22 Julai 2018
Hatua ya 32 bora....
v  1 - 24 june-Michezo  ya makundi.
v  25 june-Droo ya 16 bora mtoano.
v  27 june -4 julai-Michezo ya 16 bora mtoano.
v  2 julai-Droo ya robo fainal.
v  6 - 9 julai - Michezo  ya robo fainal.
v  9 julai- Droo ya nusu fainal.
v  14 - 15 julai-Michezo ya nusu fainal.
v  20 julai - Mchezo wa mshindi wa tatu.
v  22 julai - Fainali Ndondo Cup
Dar es Salaam
Viwanja....
v  Bandari
v  kinesi
5.
28 Julai 2018
Usiku wa tuzo za Ndondo Cup
Dar es Salaam (clouds media)




6.
18 Aug -22 Sept 2018
Ndondo Cup mkoani  Ruvuma
Songea
Mbinga
7.
5 Oct - 10 Nov 2018
Ndondo Cup Mkoani Mwanza
Mwanza
8.
15 - 22 Dec 2018
Ndondo Super Cup
Dar es salaam

NDONDO ACADEMY
Almas Kasongo-m/kiti DRFA
Pamoja na kuwepo kwa ndondo cup mwaka huu tumekusudia pia kuwepo kwa ndondo academy kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 15 kutoka vituo mbalimbali vya michezo na mashule ya jiji la  Dar es salaam.
Michezo ya mashindano haya itakuwa ikichezwa kila wikiendi na kipindi ambacho shule zitakua zimefungwa basi tutayachezesha hadi katikati ya wiki.
Usajili wake unaenda sambamba na usajili wa ndondo cup na ada yake itakua shilingi laki moja.
UDHAMINI WA mCHEZA TANZANIA
Moses Simon - Mkuu wa kitengo cha masoka-mCHEZA
NapendakuchukuafursahiikuwashukuruwaandishiwahabariwotekwakufikahapailikuwezakuwahabarishaWatanzaniakuhusuufunguzihuurasmiwamashindanohayakwamwaka 2018 kupitia UDHAMINI MNONO KUTOKA Mcheza Tanzania.
KipekeekabisaMcheza Tanzania, tunawashukuruwaandaajinawaratibuwamashidanohayayaNdondo Cup kampuniya Clouds media group kwaushirikianowa SHADAKA SPORTS MANAGEMENT chiniyausimamizimzuriwaNduguShaffihDauda, lakinibilakuwasahau TFF.
Mcheza Tanzania nikampunimpyayamichezoyakubashiriiliyosajiliwakisherianaBodiyamichezoyakubahatisha Tanzania iliyopewaLesenihalalikwaajiliyakuendeshashughulizake Tanzania.
TumekuatukiyafatiliamashindanohayayaNdondo cup kablahatahatujaanzashighulizetu, kamaMcheza Tanzania maonoyetumakubwanikuibuavipajivyavijanawaliokomtaaniambaohawajawezakupatanafasiyakuoneshavipajivyaoiliviwezekuwasaidiakuendeshamaishayao.
KwahiyotulivutiwasananaMashindanohayakwasababuyalilengakusaidiakuibuavipajivyavijanawadogokabisawaliopomtaaniambaohawakuwahikupatafursayakuvioneshavipajivyaoambavyovingewezakuwamsaadanakuendeshamaishayaokupitiavipajihivyo.Lakini pia kupunguzawimbikubwa la vijanakujihusishanamatukioyakiuharifunabadalayakewajihusishenamichezoambayokwasasaniajiranzurikabisakwavijana.
Mwaka 2017 Mcheza Tanzania tulidhaminimashindanohayakwamikoamitatuambayoni, Dar es salaam, Mwanza na Mbeya. Vipajivingitulivionanamafanikioyalikuamakubwasana.
Mwaka 2018 namiakamingineinayokujaMcheza Tanzania tumeamuakujanaudhaminimnono Zaidi ilikuongezathamaniyamashindanohaya, tunatakazawadiziwenyingikwavipengerevingitofautitofautiilikuongezamorali (motisha) kwawachezajinawashangiliaji pia.
Tunaziombatimuzotezitakazoshirikimashindanohayazidumishe Amani naupendokama FIFA wanavyosema “FAIR PLAY”
Mwishokabisa tuna wakaribishawotekujisajilinakubashirinamchezakupitiatovutiyetuya www.mcheza.co.tz kuna Odds bomba, machaguo (options) zaidiya 200 kwamechimoja, Live betting, bonasizaukweli, Malipoyapapokwahaponahudumakwawatejasaa 24 piganamba 0764701600. Jishindiemshikowakutosha,
Kwa habarimbalimbalitafadharitufatekwenyekurasazetuzamitandaoyakijamiiyotekwajina la Mcheza TZ.
Mcheza “USHINDI KOTE KOTE”



No comments: