Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akiangalia nguo zinazoshonwa na kikundi cha ushonaji kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita ambacho kimenufaika na mkopo wa shilingi milioni mbili kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri hiyo. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho ili kuona fedha za mkopo zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.
Vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka katika kijiji cha Kitigiri wakifurahia fedha shilingi 50,000/= walizopewa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) kwa ajili ya kununulia soda za sikukuu ya Krismasi . Waziri Dk. Mukangara aliwahimiza vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Geita, Kata ya Bukondo na kijiji cha Kitigiri mara baada ya kumaliza ziara yake katika kijiji hicho ili kuona fedha za mkopo za mfuko wa maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita, Enos Komanya wakati alipotembelea kikundi hicho ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri. Waziri Dk. Mukangara alitembelea
kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo zilizotolewa na mfuko wa
maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.(Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
No comments:
Post a Comment