Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiongea jambo na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo Vijana James Kajugusi (aliyevaa suti ya blue) jana mara baada ya kumaliza kuwatembelea vijana wajasiriamali wa soko kuu la jijini Mwanza ambao walipata mkopo kutoka mfuko wa vijana kupitia Halmashauri ya jiji. Waziri Dk. Mukangara aliwatembelea wajasiliamali hao ili kuona fedha walizopata zimewasaidiaje
kama kundi la vijana na kijana mmojammoja.
Mwenyekiti wa SACCOS ya Wafanyabiashara Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza (WADOKI) Mussa Ally akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia)
mfano wa jengo wanalolitarajia kujenga hivi karibuni kama kitega uchumi
chao jijini Mwanza. SACCOS hiyo ilipata mkopo kutoka mfuko wa
vijana mwaka 2009 fedha ambazo waliwakopesha vijana wanachama 12.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiongea jambo na Songaleli
Mzee (kulia) ambaye ni mfanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza
aliyepata mkopo kutoka mfuko wa vijana na kufanya biashara ya nafaka.
Katikati ni Edward Kabululu ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza
SACCOS ambayo ni moja kati ya 14 za mkoa wa Mwanza zilipata fedha za
vijana mwaka 2009 na kumpatia mkopo Mzee. (Picha na Anna Nkinda – Maelezo)
No comments:
Post a Comment