KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, January 18, 2013

ENEO LA UWANJA WA MACHAVA KIGAMBONI HATARI SANA KWA MAISHA YA WANAFUNZI WA VYUO VYA IFM NA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM.

 Mama akiwa amebeba mtoto akikatiza Uwanja wa Machava Kigamboni mchana lakini kuanzia saa 1;00 usiku usikatize eneo hili hasa kama wewe siyo mzawa au mwenyeji wa eneo hili utakabwa na kuibiwa kila kitu chunga sana kwa usalama wako.
 Mama huyu anakatiza katikati ya Uwanja wa Machava Kigamboni mchana,lakini usiku ni hatari hasa hasa kwa wanafunzi wa Vyuo vya IFM na Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
 Mtaa wa Machava wenye Hosteli (kushoto) ambazo ni makazi ya wanafunzi wa Vyuo hivyo mbele ni barabara inayoelekea Kivukoni ukipita usiku unakabwa na VIBAKA wanaokaa juu ya miti kufanya mawindo ya uharifu.
 Machava eneo hatari wakati wa usiku mchana poa tu watu wanajimwaga na zao.
 Moja ya Hosteli zinazokabiliwa na wakati mgumu wanafunzi usiku wanakimbia na kwenda kulala wanakojua ili walale kwa usalama na asubuhi wanarudi, wanaiomba Serikali na wenye nyumba kuungana ili kuhimalisha ulinzi na usalama.
 Mtaa huu usiku unageuka kuwa eneo hatari kwa kuwa kuna Hosteli hii.
 Geti hili usiku linapitika kiuraini na VIBAKA kuingia ndani na kunyang'anya vitu vya wanafunzi wa Vyuo.
 Kwenye uwa wa moja ya Hosteli Kigamboni.
 Moja ya Hosteli Kigamboni.

 Hosteli inayoangalia Uwanja wa Machava Kigamboni Dar es Salaam ambalo ni eneo hatari sana
.
Na TANZANIA LIVE BLOG
Eneo la Uwanja wa Machava Kigamboni Dar es Salaam linalalamikiwa na wanafunzi wa Vyuo vya Usimamizi wa Fedha (IFM) na Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kutokuwa salama kwa wanafunzi hao na mali zao.
Wanafunzi wengi wanaoishi katika Hosteli zinazozunguka maeneo hayo na mengine yenye Hosteli yamekuwa hatari sana kwao kuliko mtu yeyote anaeishi maeneo hayo.
Vibaka wanawafahamu wanafunzi hao hivyo basi ni rahisi kuwafanyia unyama mara tu kiza kinapoingia hasa wakati wanapotoka Chuoni muda wa saa 1;00 usiku,Vibaka hao wanakaa juu ya miti wanapowaona wanakuja wanajipanga kuwavamia na kuwapiga na kuwapola laptop,fedha na simu.
Kibaya zaidi kuna baadhi ya wanafunzi wanabakwa na wakati mwengine wanawavamia ndani ya Hosteli wanazoishi na kupelekea wanafunzi hao kupoteza muelekeo nzuri katika masomo yao.
Wameiomba Serikali na wamiliki wa nyumba zenye Hosteli kuweka walinzi Sungusungu ambao watawalipa kutokana na tozo la kodi wanazolipa ili kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo kwa nyakati za mchana na usiku.   

 

No comments: