Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Esther Mkwizu (kulia) akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Salim Ahmed Salim (wapili kushoto) akizungumza katika mkutano na Viongoziwa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Mwenyekitiwa Chama cha Kijamii (CCK), Constantine Akitanda( wa tatu kushoto) akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya Chama hicho kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Riziki Mngwali akizungumza katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam baina ya Tume hiyo na Chama cha Wakulima (AFP), wakati ujumbe wa Chama hicho ulipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume ya Mabadilikoya Katiba, Mhe. Raza Hamad (kushoto) akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Wakulima (AFP) uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP), Rashidi Mohamed (kulia) akiwasilisha maoni yao kuhusu Katiba kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) waliofika katika Ofisi za Tume hiyo kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Wapili kulia ni Katibu wa Tume, Assa Rashid na kushoto ni Viongozi wa Chama hicho, Juma Shariff na Moshi Kigundu.
Baadhi ya Viongoziwa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) wakifuatilia mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambapo Uongoziwa Chama hicho uliwasilisha maoni ya Chama hicho kuhusu Katiba Mpya.
1Katibu wa
Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), Juma akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika baina ya Chama hicho na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambapo
Chama hicho kiliwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya .Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo,
Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume,Assaa Rashid.(PICHA NA TUME YA KATIBA)
No comments:
Post a Comment