Mama huyu akiwa amelala kwa kuegemea ndoo akisubili Samaki
Kinamama wakisubiri samaki.
Muuza samaki akiwanadi samaki.
Mama akitoa fedha kununua samaki ambao amelipia tsh 9500.
Na TANZANIA LIVE BLOG
Kipindi hiki ni kigumu kwa upatikanaji wa samaki katika Bahari ya Hindi, Kutokana na hali hiyo samaki hawapo wengi kama ilivyozoeleka katika Soko la Feri Dar es Salaam.
Kinama hawa pichani wanasubili samaki ambapo hao kidogo wanauzwa kwa bei mbaya sana dagaa uuzwa kwa tsh 4500 wasiozidi kumi.
Kwa mujibu wa mmoja wa wavuvi amesema hali hii imeanza juzi na inakadiliwa kuishi kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Kinamama hawa wamesema kuwa hali ni mbaya kwao kiuchumi kwani mategemeo yao ni kupata samaki na kuuza ili maisha yao kila siku na familia zao yaweze kwenda.
No comments:
Post a Comment