KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Monday, January 21, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

                                                         21 Januari, 2012

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizotolewa na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kuhusu pembe za ndovu, kama ilivyoelezwa katika gazeti la Nipashe toleo namba 057638 la Januari 21, 2013, Mtanzania toleo namba 7206 la Januari 21, 2013 na Tanzania Daima toleo namba 2737 la Januari 21, 2013.

Anayeshikiliwa na Polisi kwa mahojiano ya tuhuma hiyo ni MT 59509 Sergent Azizi Athuman Yusufu, ifahamike kwamba gari linaloshikiliwa na Polisi ni gari la Serikali lenye namba za usajili STK 3216 ambalo hutumiwa na mkufunzi wa Kijeshi kutoka Zimbabwe anayefundisha hapa nchini ambaye hakuwemo katika gari hilo siku ya tukio la ajali na upekuzi ulipofanywa.  Ifahamike kuwa anayeshikiliwa ni askari mtajwa na siyo Mwambata Jeshi kama Vyombo vya Habari vilivyoeleza awali, hali iliyoleta usumbufu kwa mwambata wa Zimbabwe aliyepo hapa nchini, baada ya kuona anatuhumiwa katika vyombo vya habari akiwa hajui chochote kuhusiana na tukio hili.

Kwa taarifa za ziada wasiliana kupitia - simu No: 0764-742161.

No comments: