Waziri mkuu Mizengo Pinda akipokewa na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo kuangalia shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Ofisi hiyo Dar es salaam.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu matumizi ya ramani
katika upataji na ukusanyaji wa takwimu mbalimbali zinazotumiwa katika
masuala mbalimbali nchini kutoka kwa Kaimu Meneja wa Idara ya Mbinu za
Kitakwimu, Viwango na Uratibu Bw. Emilian Karugendo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
(kulia)akimfafanulia jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) kuhusu
takwimu za Kilimo na uchumi. Kushoto kwa waziri Mkuu ni Waziri wa Fedha
Dkt. William Mgimwa.
Waziri mkuu Mizengo pinda (kulia katikati) akitazama takwimu mbalimbali
alipotembelea kitengo cha ramani akiwa na Waziri wa Fedha na Uchumi
Dkt. William Mgimwa (kushoto), Dkt. Albina Chuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (kulia).
Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu Vincent Mgaya
(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu matumizi
ya ramani kupata Takwimu za Kilimo, Uchumi na Utalii.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimweleza jambo Meneja wa Takwimu za Kilimo
Bi. Joyce Urassa alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dar es
salaam.
Meneja wa Idara ya Pato la Taifa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Daniel
Mwasula akitoa ufafanuzi kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusu Pato la
Taifa na namna ofisi yao inavyofanya kazi kukokotoa pato la Taifa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika Picha ya Pamoja na viongozi na
watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kukamilisha ziara
yake.
No comments:
Post a Comment