Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za
bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa bunge
uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya
kamati kuondolewa pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3
zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bajeti na Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Thomas Kashililah akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu
wa wabunge kuzisoma na kuzitumia ipasavyo kanuni za bunge ili kuondoa
manug'uniko yanayojitokeza pindi wanapozuiliwa na spika kuchangia
mijadala au kutoa hoja bungeni kwa sababu ya kukiuka kanuni na umuhimu
wa waandishi wa habari kuzitumia taarifa rasmi za bunge
katika utoaji wa taarifa zao.
Waandishi wa habari wakiendelea kupata ufafanuzi wa
masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za Bunge kutoka kwa Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, Dar es salaam. Pamoja na
mambo mengine amesema ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vya
habari katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bunge pamoja na uandaaji
wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge. (Picha na Aron Msigwa - MAELEZO).
No comments:
Post a Comment