Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa leo jijini Dar es salaam.
Waziri
mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa
kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za
Atomiki Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya lenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia
wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa leo Ocean Road jijini Dar es
salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof.
Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road
Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.
Waziri
mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni
mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa
wa kansa katika Hospitali ya Kansa Ocean Road kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.
Baadhi ya wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road wakiwa ndani ya moja ya chumba cha jengo
jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine yenye
uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na
Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini
Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa
Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia
wa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za
Atomiki Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu
zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo
wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini
Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya
Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania huku shirika hilo likitoa msaada wa mashine mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa binadamu. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).
No comments:
Post a Comment