Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT)
unafanyika Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa,
tofauti na taarifa wanazopewa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro keshokutwa (Februari
12 mwaka huu) . Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za
uanachama kwa mwaka 2013 kabla ya uchaguzi.
Wagombea
ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.
Abdallah
Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi
ya Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati
nafasi ya uwakilishi wanawake yupo Isabela Kapera.
Wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment