Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaka washabiki wa mpira wa miguu
kujitokeza kwa wingi wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simba
zitakazocheza mechi za mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.
Nguvu
ya washabiki ni muhimu katika kuziweza timu hizo kufanya vizuri katika
mechi hizo za nyumbani dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club
Libolo ya Angola.
Azam
itacheza Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katika
mechi ya Kombe la Shirikisho wakati Simba itaikabili Club Libolo kwenye
mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Jumapili. Mechi zote
zitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
LYON, YANGA KUUMANA UWANJA WA TAIFA
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inamaliza raundi
ya 16 kesho (Februari 13 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji African
Lyon dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo itakayochezshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro
inakutanisha timu zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo
vinara wa ligi hiyo kwa pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na
Salum Bausi inakamata mkia ikiwa na pointi tisa tu.
Nayo
Toto Africans itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob
Adongo kutoka Musoma. Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wa
kuchukua watazamaji 20,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo
Shooting na Oljoro JKT.
Nahodha
wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha wa Mtibwa
Sugar ataiongoza timu yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting
kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo
huo ambapo Mtibwa Sugar katika mechi yao iliyopita walichapwa mabao 4-1
na Azam.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment