Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo akiwafundisha maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi, wakala, mashirika ya Umma, mikoa na wilaya upigaji wa picha bora za mnato kwa matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maafisa hao mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement
Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha
maafisa habari na mawasiliano wa serikali akiongea na mafiasa hao mjini
Dodoma.
Naibu
katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.
Sihaba Nkinga akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha mafisa
habari wa Serikali katika kampasi ya chuo kikuu Dodoma.
Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.
Mhasibu
mkuu msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.
Swalehe Chondoma akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya
chuo kikuu cha Dodoma.
Maafisa
habari na mawasiliano wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Maafisa
Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maafisa
Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maafisa
Habari na Mawasiliano wa serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma
kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya
mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho.
Baadhi
ya viongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw.
Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Habari Usajili wa Magazeti Bw. Raphael Hokororo (wa pili kutoka kushoto)
wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa
wabunge mara baada ya kuombwa na Mh. Spika wakiwaongoza maafisa habari wa serikali.
Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).
No comments:
Post a Comment