OFISA
Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi amewasili leo kwa ajili ya kufuatilia
shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Mamelodi,
ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za maendeleo nchini Tanzania
tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, pia amekuja kumtambulisha
msaidizi wake, Patrick Onyango aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi
karibuni.
Wakiwa
nchini, wawili hao wanatarajiwa kupata taarifa ya maendeleo ya mradi wa
kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, baada ya
FIFA kuipa Tanzania mradi wa nne (GOAL Project 4) wa kuweka miundombinu
kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu.
Mwanza
ilipata mradi huo baada ya Halmashauri ya Jiji hilo kukubali masharti
ya mradi huo ya kulipia nakisi ya fedha zinazolipwa na FIFA, ambazo ni
sh. milioni 700. Mradi huo wa kuweka nyasi bandia Nyamagana utagharimu
sh. milioni 900, hivyo nakisi y ash. milioni 200 italipiwa na Jiji la
Mwanza.
Pia
Mamelodi na Onyango watapata taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa
Gombani uliowekwa nyasi za bandia kwa msaada wa FIFA katika mradi wa
GOAL Project 3; na pia kupata mikakati ya maendeleo ya TFF kwa mwaka
2013, ikiwa ni pamoja na kozi na semina mbalimbali zitakazofanyika
nchini mwaka huu.
Mamelodi
na Onyango pia watapata taarifa ya maendeleo ya uboreshaji wa
mashindano ya Copa Coca-Cola baada ya FIFA kuingia rasmi kwenye
mashindano hayo mwaka jana kwa kuendesha kozi kwa walimu wa timu za
kombaini ya mikoa na waamuzi.
Kwa
sasa mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka
17, lakini FIFA inataka yahusishe umri mdogo zaidi ili kuendeleza soka
ya vijana na kushirikisha kikamilifu shule. Maofisa hao wataondoka
nchini Jumatatu asubuhi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment