Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata ujumbe kupitia simu za mkononi ambao umesambazwa kwa
wananchi mbalimbali ukisadikishwa kuwa unatolewa na JWTZ. Ujumbe huo wa simu ya
mkononi unasema ‘Habari
zilizotufikia hivi punde. Mtanzania yeyote, kaa makini usiokote kitu chochote
ambacho una shaka nacho, kunabomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya
30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la
chai chenye rangi ya fedha. Usiguse’
Piga namba
0756 000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo. Imetolewa na JWTZ’.
JWTZ linapenda kuwaondoa wananchi hofu kutokana
na taarifa hiyo. Kwanza, Ujumbe huo haujatolewa na JWTZ. JWTZ haliwezi likatumia mfumo huo wa SMS kuwapa
wananchi wake taarifa za hatari kama hizo. Aidha, JWTZ hutangaza kupitia vyombo
rasmi kama vile Magazeti, Radio na Television.
Pili, bomu la tani 100 ni zito mno, halijawahi kutengenezwa duniani. Na kama lipo,
haifahamiki bomu hilo litarushwa vipi , kwa kutumia ndege au
Mzinga?. Lakini
pia, mzinga wa aina hiyo haupo duniani kote na wala hakuna ndege yenye uwezo
huo, hasa kwa bomu lenye umbile dogo kama hilo(Chupa ya Chai).
Tatu, habari hizi hazina ukweli kisayansi wala kiuhalisia
au fikra za kawaida. Tunawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizi kwani sio za
kweli ni uongo mtupu. JWTZ lipo kwa ajili ya Wanachi hivyo, kwa taarifa hizi za
hatari,lazima lingewajulisha wananchi kwa njia zilizoelezwa hapo juu na si kwa
simu za mkononi.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment