Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mfalme Mswati wa Swaziland na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Benard Membe wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais Kikwete kwa Marais na wajumbe wa mkutano wa smart partnership unaofanyika Dar es Salaam
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akijiandaa kuzungumza na wake wa Marais na Wakuu wa nchi wakati wa mkutano wa smart partnership kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mke wa Mfalme wa Mswati wa Swaziland, Inkhosikati Lambikiza (kushoto), na Mwakilishi wa Mke wa Rais Joseph Kabila wa DR Congo (kulia) wakimwalika Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott (hayupo pichani) kujiunga nao katika picha ya pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi wanaohudhuria mkutano wa smart partnership unaofanyika hapa Dar es Salaam. Kutoka kushoto no Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia akifuatiwa Inkhosikati Lambikiza, Mke wa King Mswati, Mama Salma Kikwete, akifuatiwa na Mama Siti Hasma, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Malasya Mahathir Mohammed na kulia ni mwakilishi wa Mke wa Rais wa DR Congo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mama Siti Hasma mara baada ya kuhudhuria kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi kwenye mkutano wa smart partnership.
Mke wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland.
Mama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wkijiandaa kwenda katika chakula cha usiku kilichoandaliwa kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Inkhosikati Lambizana kwenye ahckula cha usiku.
Waziri Mkuu wa Malasya Mheshimiwa Najib Razak akiwa pamoja na Mama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wakimwangalia simba dume aliyewekwa nje ya ukumbi wa jengo la mikutano la Mwalimu Nyerere baada ya viongozi hao kuhudhuria chakula cha usiku.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mfalme Mswati wa Swaziland mara baada ya chakula cha usiku.
Rais Jakaya Kikwete akiiagana na Waziri Mkuu wa Malasya Mheshimiwa Najib Razak mara baada ya viongozi hao kupata chakula cha usiku kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.(PICHA NA JOHN LUKUWI)
No comments:
Post a Comment