KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, June 28, 2013

MAONYESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YAMEANAANZA KABLA YA USAFI,UJENZI WA BARABARA NA MAJENGO KUWEKA RANGI KUKAMILIKA NA WENGINE KUZUIWA KUINGIZA VIFAA VYA KUMALIZIA UJENZI.

 Mlango mkuu wa kuingilia Viongozi ndani ya Uwanja wa Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Barabara ya Kliwa bado haujaandikwa kwa juu kama ilivyozoeleka miaka yote.
 Banda la Polisi ndiyo kwanza linapakwa rangi katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba.
 Fundi wa kuchora akiendelea na kazi wakati maonesho yakiendela.

 Moja ya mti uliokatwa ukielea ndani ya Uwanja wa Maonesho pamoja na kuanza. 
 Ujenzi wa moja ya Banda ukiendelea ndani ya Uwanja wa Sabasaba barabara ya Kilwa.
 Mmoja wa washiriki wa Maonesho akiwa amebeba kiroba cha nafaka.
Uchafu kama kazi ndani ya Uwanja wa Sabasaba kama unavyoonekana huku maonesho hayo yakiwa yameanza.
Banda la Kampuni ya Simu ya Vodacom bado likiendelea kujengwa.Vodacom ni wadhamini Wakuu wa Maonesho haya ya 37 lakini wamekuwa katika wakati mgumu kuingiza vifaa vya kumalizia ujenzi wa Banda lao kwani wanapopita mlango mkuu wanazuiwa kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wao.
 Uchafu uliorundikwa eneo la Banda la Kampuni ya simu Tanzania.
 Barabara zilizomo ndani ya Uwanja wa Sabasaba ni mbovu zinabomolewa siku ambayo maonesho yameanza.
Kibarua akichimba lami na sululu ili iwekwe lami ndani ya Uwanja wa Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
 Kibarua akichimba na sululu.
 Mafundi wa ujenzi wakikata lami kwa mashine ili kuweka kalaka tayari kuweka lami katika eneo la Banda la kufungua Maonyesho.

 Mkusanyiko wa takataka katika moja ya barabara zilizomo ndani ya Uwanja wa Maonyesho.
Kibarua akichimba lami kwa sululu na kuweka viraka kabla kuweka lami ndani ya Uwanja wa Maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa Barabara ya Kilwa.(PICHA NA TANZANIA LIVE BOLG)

No comments: