Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya
Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya
kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huo. Wa pili kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison
Mwakyembe (wa tatu) kulia.
 Mojawapo ya vivutio vikubwa katika jiji la Singapore ni hoteli hii ya 
kitalii na casino iitwayo Marina Bay ambayo kuna jengo la mgahawa  lenye
 umbo la meli juu ya majengo yake mawili. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao 
makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya  ya Singapore ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa 
mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa 
mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya 
Elimu  ya ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA 
kwa Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine walijionea 
jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali 
ikiwa ni pamoja na vya ndege.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na 
viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea 
kampasi yao jijini Singapore.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao 
makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi 
kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji 
ya muda mfupi na muda mrefu.

makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore,ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi 
kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji 
ya muda mfupi na muda mrefu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa miji ya Singapore.(PICHA NA IKULU).

No comments:
Post a Comment