Mtoto Faith Warioba nayesoma katika shule
ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda
Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya
Kikwete akishuhudia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na
mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili
nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na
Msaidi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia Balozi Liberata Mulamula wakati Rais
Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa
mgeni wake muda mfupi baaday kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni
wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda
mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere.
Rais Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride
la heshima liliandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda
mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni
wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya
ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati
alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni
wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya
ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati
alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.(Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment