KAMANDA WA POLISI
[M] DODOMA
TAARIFA YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO
VYA HABARI TAREHE 21/06/2013
Mnamo
tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs maeneo ya Area ‘E’ Manispaa ya Dodoma
Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia
NCCR – Mageuzi wakati anaelekea nyumbani kwake anakoishi njiani alikutana na
vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga honi lakini
hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya barabara si
nitawagonga?” Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya motto wa Mbunge, tutakupiga
sasa”.
Alipojaribu
kupita walipiga gari lake. Ilimbidi ashuke ili atazame kama gari hilo limepata
uharibifu. Ndipo vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye
akijitahidi kujihami, ndipo wakatokea vijana wawili (2) na kumsaidia. Kijana
mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni
kijana aliyekuwa anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.
Watuhumiwa
baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Mheshimiwa Machali aligundua
kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo.
Msako
mkali ulifanyika na usiku wa manane watuhumiwa wawili (2) walikamatwa ambao
ni:-
1.
JEREMIA S/O LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka
18, Mkaguru, Mkulima, Mkazi wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. Huyu amekutwa akiwa
na jeraha usoni alilopata wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana
waliokuwa wanamsaidia.
2.
CHARLES S/O CHIKUMBILI, Miaka 22,
Mkulima, Mkazi wa Swaswa, Manispaa ya Dodoma.
Watuhumiwa
walipokamatwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi.
No comments:
Post a Comment