Eleuteri Mangi –Maelezo,Dar es Salaam.
KAMPUNI ya mbegu ya TANSEED International yenye makao makuu mjini Morogoro imeandaa maonesho ya shamba darasa ya teknolojia mpya ya mbegu za mahindi ya TAN 222 kukomesha kiduha “trigaway maize”kwa ajili ya kudhibiti magugu hatari ya kiduha kwenye zao la mahindi.
KAMPUNI ya mbegu ya TANSEED International yenye makao makuu mjini Morogoro imeandaa maonesho ya shamba darasa ya teknolojia mpya ya mbegu za mahindi ya TAN 222 kukomesha kiduha “trigaway maize”kwa ajili ya kudhibiti magugu hatari ya kiduha kwenye zao la mahindi.
Maonesho hayo yatafanyika kesho (Jumamosi) katika maadhimisho ya siku ya wakulima (Farmer
Field Day) katika kijiji cha Mkuza
wilayani Mheza ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku
Galawa.
Ambapo yatahudhuriwa na watafiti wa mazao ya kilimo, wataalamu wa ugani,
makampuni ya mbegu, wakulima, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali mkoani humo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Isaka Mashuri leo jijini Dar
es salaam katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari -MAELEZO
alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani
Tanga.
Alisema lengo la maonesho hayo ni kuhamasisha
wakulima, watafiti, washauri wa ugani, wasiasa, taasisi za serikali na zisizo
za kiserikali pamoja na wadau wengine ni kuhusu tishio linatokana na magugu ya
kiduha.
“Magugu ya kiduha yamekuwa ni
tatizo kubwa kwa wakulima wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kipindi
cha miongo saba. Kiduha ni magugu tegemezi yanayojishikiza kwenye mizizi ya
mazao ya nafaka na kunyonya maji , madini
na virutubisho vingine.” alisema Mashuri.
Mashuri aliongeza kuwa magugu hayo huharibu ya mahindi kwa kutoa
sumu na kuweza kuangamiza mimea ya mazao hata kabla magugu hayajajitokeza juu
ya ardhi.
“Magugu ya kiduha huzaa mbegu
nyingi kati ya 5,000 hadi 200,000 kwa mmea mmoja, hivyo kufanya tatizo kuwa
kubwa zaidi kwani mbegu za kuduha huweza kubaki zikiwa hai aridhini kwa muda mrefu zaidi ya miaka 20 na
zaidi na kusababisha upungufu wa chakula kila mwaka, ” alisema Mashuri.
Alisema kwamba inakadiriwa kuwa takribani
hekari milioni 1.5 za ardhi Afrika Mashariki zimeathiriwa na magugu ya kiduha
ambapo aliitaja mikoa iliyoathirika
Tanzania na magugu hayo ni pamoja na Morogoro, Pwani , Tanga, Dodoma,Singida,
Tabora, Shinyanga , Mwanza, Mara, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Lindi na Mtwara
na kubainisha kuwa ni zaidi ya ekari 1,500,000 zimeathirika.
Aidha Mashauri alieleza kuwa magugu hayo husababisha upotevu wa mavuno
takribani tani milioni 1.7 za nafaka
zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 356 ambazo ni sawa na Sh.bilioni
584.6 za Kitanzania kwa mwaka.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la
BASF Nchini Kenya linalojishughulisha na shughuli za madawa ya kilimo, Sammy
Wairuingi alisema kuwa Tanzania tushangilie kwa furaha ya kuja kwa fursa hii ya
teknolojia mpya kwani itasaidia kuzalisha chakula cha kutosha kulisha familia ,kufukuza
njaa na umasikini.
No comments:
Post a Comment