Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
Mimba za utotoni zimeelezwa kuwa ni kikwazo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa nchi masikini ikiwemo Tanzania.
Akitoa taarifa ya siku ya Idadi ya Watu Duniani leo mjini Zanzibar,
kwa niaba ya waziri wa Fedha wa SMZ Omari Yusufu Mzee, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Zanzibar Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini, amesema mimba hizo
zimekuwa zikiathiri mipango ya kimaendeleo kwa nchi masikini.
Amesema Tanzania
ikiwa miongoni mwa nchi za bara la Afrika zenye idadi kubwa ya
wasichana wanaopata mimba za utotoni wakiwa shuleni na wale wasiosoma,
imebaini kuwa mamba hizo ni kikwazo katika mipango ya maendeleo ya
uchumi mikoani.
Amesema kwa mfano Zanzibar,
wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wenye umri kati ya miaka 12
na 18 wamekuwa wakiacha masomo kutokana na kupata mimba wakiwa shuleni.
Amesema
nyingi ya mimba hizo zimekuwa zikipatikana pasipo matarajio na mipango
kwa watoto hao ambao wameingia katika kundi la wazazi ambapo amesema ni
matokeo ya kuanza ngono utotoni zisizo salama.
Dr.
Mwinyihadi amesema mimba za utotoni humkosesha mtoto wa kike elimu ya
lazima na kumdumaza kimaisha wa kuanza mapambano mapema ya kujitegemea
binafsi kimaisha na kuzorota kwa ukuaji wa kiuchumi kwa taifa.
Amesema
pamoja na taarifa za wasichana 8,000 kuacha shule kila mwaka hapa
nchini kwa mimba, lakini idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wasichana
wanaoozeshwa na wazazi wao kwa watu waliowafanyia ukatili wa kingono.
Amesema katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2008 hadi 2012, wasichana 659 waliacha masomo katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba ambapo kati ya hao, watoto 277 waliacha masomo kutokana na ujauzito na wengine 382 waliolewa wakiwa shuleni.
Hata
hivyo Dr. Mwinyihadi amesema ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa
mtoto wa kike, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha vituo
vijulikanavyo kama Mkono kwa Mkono katika mikoa ya Unguja na Pemba
ambapo yeyote anayefanyiwa ukatili wa kijinsia hutoa ripoti na hatua
kuchukuliwa kwa mkosaji.
Amesema hatua hiyo
imewafumbua macho wananchi na hata kupunguza kwa kiasi kikubwa vitendo
vya unyanyasaji kwa mtoto wa kike visiwani humo.
No comments:
Post a Comment