NA JENNIFER CHAMILA
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
Mohammed Gharib Bilal amewataka
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi
kuweza katika mkoa wa Tabora kwa kutumia rasilimali zilizopo katika sekta
mbalimbali mkoani humo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Makamu wa Rais Dk. Bilal wakati
akifungua Kongamano la Uwekezaji la Mkoa wa Tabora liliofanyika kwenye hoteli
ya Serena jijini Dares Salaam,ambalo limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo
wawekezaji, wadau wa maendeleo, wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo.
Makamu wa Rais , Dk.
Bilal aliwataka wawekezaji hao kuwekeza kwa kutumia rasilimali ambazo ni asali, madini,maeneo ya kihistoria, ujenzi wa
hoteli,sehemu za kupumzika, viwanja vya michezo gofu, usafiri nchi kavu na
angani,ufugaji wa wanyama wa porini,kampuni za kitalii, uwindaji wa wanyama,
vivutio vya kiutalii vya kiutamaduni na
kihistoria.
“Serikali inawahamasisha wawekezaji wa sekta binafsi na
wawekezaji ambao watashirikiana na Serikali katika maeneo hayo,” alisema Dk.
Bilal.
Dk. Aliongeza kuwa milango iko wazi kwa uwekezaji wa miundombuni
ambayo, barabara kubwa, madaraja,
mwasiliano ya simu, viwanja vya ndege, usambazaji miundombinu ya maji, hivyo wawekezaji kutoka nje ya nchi
wanaruhusiwa kuwa umiliki wa zaidi ya asilimia 100 mipango ya kuhamisha na
ujenzi inaruhusiwa kupitia maeneo hayo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Fatma
Mwassa alisema wahahitaji shirikiano wa uwekezaji huo na kukuza masoko na tayari
wameshaandaa mazingira mazuri.
“Ardhi tunayo tumeshaipima,tunahitaji wawekezaji katika
kilimo, mafuta , nyama, maziwa na madini,” alisema Fatma.
Naye Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta alisema mkoa huo umepata kiongozi mzuri na watendaji
na umejipanga ipasavyo juu ya jambo hilo.
“Kuanzia sasa mtumishi anapimwa kwa matokeo ya kazi yake .
Tusiwe tunalalamika sisi ni masikini
tutumie fursa zilizopo ili kuondoa umaskini kinachotakiwa ni uongozi usimamizi
bora ili kuondokana na umaskini,” alisema Waziri Sitta.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC),
Julieth Kairuki alisema taasisi hiyo
imejipanga vizuri ili kusaidia uwekezaji katika mkoa huo na itaweka vituo
mbalimbali.
Aliongeza kuwa hivi sasa kunawawekezaji 36 waliojitokeza
kuwekeza kabla ya kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment