Mchoraji katuni, Nathan Mpangala,
ambaye pia ni mwanzilishi na mratibu wa marafiki wa Wafanye Watabasamu,
akiwaelekeza baadhi ya watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Dar es Salaam, leo walipowatembelea ili kuwajulia hali, kuwapa zawadi kisha kuchora
nao. Wafanye Watabasamu ni mkusanyiko wa marafiki ambao hutembelea watoto
waliolazwa mahospitalini kwa kipindi kirefu ambapo huwawezesha watoto hao
kuchora michoro mbalimbali ikiwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia. (Picha kwa
hisani ya Wafanye Watabasamu)
Wachoraji katuni, Nathan Mpangala
(kulia) na Abdul King O, wakiwaelekeza baadhi ya watoto waliolazwa katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, leo walipowatembelea ili kuwajulia hali,
kuwapa zawadi kisha kuchora nao. Zoezi hilo lililofanyika chini ya mwamvuli wa
mradi wa Wafanye Watabasamu, uliobuniwa na Mpangala, ni mkusanyiko wa marafiki
ambao hutembelea watoto waliolazwa mahospitalini kwa kipindi kirefu ambapo
huwawezesha watoto hao kuchora michoro mbalimbali ikiwa ni sehemu ya tiba ya
saikolojia. (Picha kwa hisani ya Wafanye Watabasamu)
No comments:
Post a Comment