Na Frank Geofay-Jeshi
la Polisi,Windhoek Namibia.
Timu ya Polisi Tanzania
inayoshiriki Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO)
nchini Namibia imelazimishwa sare ya mabao 2 kwa 2 katika mwendelezo wa michezo
hiyo.
Mchezo huo ambao
ulichezwa katika uwanja wa Sam Njoma nje kidogo ya jiji la Windhoek ulikuwa
mkali huku Tanzania ikitawala katika vipindi vyote lakini ikishindwa kutumia vizuri
nafasi walizozipata.
Mabao ya Kongo
yalifungwa katika kipindi cha kwanza na Makundi Kaluma na Kalumba Banza na ya
Tanzania yalifungwa na Ahmed Bello kipindi cha kwanza na John Kanakamfumu
kipindi cha pili kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa kongo
kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Huu ni mchezo wa pili
kwa timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania kucheza baada ya mchezo wa kwanza
kukubali kichapo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa Zambia.
Katika Mpira wa pete
timu ya Polisi Tanzania iliweza kuifunga Angola 61 kwa 13.huku ikitoka sare na
wenyeji Namibia kwa kufungana mabao 29 kwa 29 huku ikifungwa na Swaziland 35
kwa 25.
Matokeo mengine katika
mpira wa miguu ni pamoja na Zambia 2
Lesotho 0, Namibia 1 South Afrika 0.
Timu ya mpira wa miguu
ya Tanzania itashuka dimbani tena kesho kupambana na Angola ambapo pia
wanariadha wanne wataiwakilisha Tanzania katika mbio fupi za kilometa 25.
No comments:
Post a Comment