YOSO LINDI SOCCER ACADEMY AFARIKI DUNIA
Marehemu
Exavel Richard (wa kwanza kushoto waliokaa mbele), akiwa katika picha
ya pamoja na kikosi cha Lindi Soccer Academy (LSA) nje ya Hotel Double
M, ilikokuwa imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Copa Coca Cola mwezi
uliopita. Kushoto (waliosimama) ni Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba
alipotembelea kambi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Hafidh Karongo na Meneja
wa Double M aliyekaa mbele yake.
LINDI, Tanzania
Kabla
na baada ya mazishi ya Exavel, wadau, viongozi, wachezaji na wazazi wa
wachezaji wa LSA wanakutana katika Hoteli ya Double M mjini Lindi,
kuratibu shughuli za mazishi hayo yaliyofanyika kwenye Makaburi Msafa
saa 10 alasiri jana
TIMU ya Lindi Soccer Academy (LSA) ya mjini Lindi, imepata
pigo kutokana na msiba wa ghafla wa mchezaji wake Exavel Richard, aliyefariki
jana jioni katika Hospitali ya Sokoine, alikokuwa amekimbizwa kwa matibabu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa LSA, Hafidh Karongo, Exavel
aliyekuwa tishio katika nafasi ya ulinzi wa kushoto, kiungo-mkabaji na winga wa
kushoto, alikutwa na mauti katika hospitali hiyo ya mkoa, alikokimbizwa baada
ya kulalamika maumivu ya kichwa.
Karongo alibainisha kuwa, baada ya Jumanne jioni kurejea
kutoka shule, Exavel alidai kuumwa kichwa, maumivu yaliyoendelea hadi Jumatano,
ambapo alikimbizwa hospitalini hapo na kufariki saa chache baadaye.
“Alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi
Wailes, ambapo Jumanne alikuwa na testi kujiandaa na mitihani ya taifa, alirejea
nyumbani huku akidai kuumwa kichwa, ambapo asubuhi ya Jumatano alikimbizwa
hospitali alikofariki,” alifafanua Karogo.
Exavel ambaye mechi yake ya mwisho kuichezea LSA ni ile ya
kirafiki dhidi ya Mkwaya Boys iliyopigwa Agosti 11, ambayo alicheza kwa dakika
30, atakumbukwa kwa mchango wake katika mechi 32 alizoichezea, akibeba mataji
matatu likiwamo la Lindi Street Soccer.
Kabla na baada ya mazishi ya Exavel, wadau, viongozi,
wachezaji na wazazi wa wachezaji wa LSA walikutana katika Hoteli ya Double M
mjini Lindi, kuratibu shughuli za mazishi hayo yaliyofanyika kwenye Makaburi
Msafa saa 10 alasiri jana.
No comments:
Post a Comment