Na Anna Nkinda Maelezo, New York
Chuo Kikuu cha Monmouth cha mjini New Jersey nchini Marekani kimeahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa mafunzo kwa wauguzi ili kuweza upunguza tatizo la vifo vya kina mama wajawazito na watoto nchini.
Hayo yamesemwa jana na Rais wa chuo hicho Dk. Paul Brown wakati akiongea na ujumbe maalum kutoka Tanzania ulioongozwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete uliotembelea chuo hicho.
Dk. Brown alisema wakufunzi kutoka chuo hicho watatoa mafunzo kwa makundi ya watu wachache wachache kwa njia ya kubadilishana uzoefu wa kazi (Exchange Program) ambao wataenda kuwafundisha wenzao hii itakuwa ni pamoja na wataalamu kutoka chuo hicho kuja nchini na kuwafundisha manesi au manesi kwenda katika chuo hicho kujifunza.
“Tunaomba mtupatie mtaala wa
masomo mnaotumia kuwafundishia wauguzi katika vyuo vyenu ili tuweze
kuupitia kama kuna mahali pa kuboresha tutaboresha, tutaboresha na kuutumia wakati wa kufundishia”, alisema Dk.
Brown.
Mafunzo mengine yatakafundishwa ni kwa njia ya CD na mtandao (Skype) jambo ambalo litawafanya wakufunzi pamoja na wanafunzi kuweza kubadilishana utamaduni wa nchi zote mbili pia chuo hicho kitatoa ufadhilii wa masomo kwa watu watakaosomea fani ya uuguzi.
Chuo hicho pia kimemkabidhi Mhe. Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) vitabu
4000 ambavyo vitatumika kufundishia katika vyuo vya elimu ya juu hapa
nchini kwa ajili ya masomo mbalimbali yakiwemo ya sayansi katika fani za uuguzi
na fizikia .
Kwa upande wake Mama Kikwete aliushukuru
uongozi wa chuo hicho kwa vitabu walivyowapatia na kuamua kushirikiana na
Serikali ya Tanzania kupunguza tatizo la vifo vya kina mama wajawazito na
watoto pia aliwaomba washirikiane katika ufanyaji wa tafiti mbalimbali .
“Vitabu mlivyotupatia vitapelekwa katika
vyuo vilivyokusudiwa, naamini ushirikiano huu tuliouanzisha utatusaidia
kujiendeleza katika mambo mbalimbali na kufikia malengo tuliyojiwekea”, alisema
Mama Kikwete.
Naye waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.
Hussein Mwinyi alisema Serikali imejitahidi kuboresha huduma ya afya kwa
wananchi wake na kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto
wachanga vinavyotokea wakati wa kujifungua vinapungua na hadi sasa vifo hivyo
vimepungua kutoka 578 kwa kila vizazi hai 100000 hadi kufikia 454.
“Vifo vingi vya kina mama wajawazito na
watoto vinavyotoea wakati wa kujifungua vinatokana na upungufu wa wataalamu wa
afya tulionao wakiwemo wauguzi hivyo basi tunaomba tushirikiane katika hili ili
muweze kutusaidia kutoa elimu ya ukunga na uuguzi kwa watu watakaohitaji kusoma
fani hii”, alisema Dk. Mwinyi.
Alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2004 hadi asilimia 5.1 kwa mwaka 2011.
Alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2004 hadi asilimia 5.1 kwa mwaka 2011.
Chuo cha Monmouth baada ya kusikia kazi
zinazofanywa na Taasisi ya WAMA moja wapo ikiwa ni kuboresha afya ya mama
wajawazito na watoto waliamua kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo
la afya.
Mama Kikwete ameambatana na mmewe Mhe.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa
68 wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN).
No comments:
Post a Comment