Taarifa hii yahusu zoezi la utoaji vitabu vya sheria kwa vyuo
vikuu mbalimbali vinavyofundisha masomo ya sheria hapa nchini. Kampuni ya LawAfrica ambayo inafanya shughuli za kibiashara za
uchapishaji na usambazaji wa vitabu vya sheria katika nchi za Africa mashariki
imeamua kutoa msaada wa vitabu mbalimbali vya sheria katika vyuo mbalimbali vya
elimu ya juu ili kuweza kuchangia juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali na
wadau wengine katika kuboresha taaluma hii muhimu hapa nchini. Malengo mengine
ya zoezi hili ambalo litakuwa endelevu ni kama yafuatayo:
1. Kuhamasisha
wachapishaji wengine kutoa misaada ya vitabu katika sekta ya elimu na katika
ngazi tofauti yaani katika ngazi ya shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu
2. Kuhamasisha
wadau wengine kuchangia sekta ya elimu kwa kutoa misaada ya vitabu ambavyo ndio
vitendea kazi vikuu kwa walimu katika kufundisha na wanafunzi pia katika kujifunza.
3. Kutoa
changamoto kwa wanafunzi na pia kwa watanzania wote kiujumla kujenga mazoea ya
kujisomea vitabu. Tabia ya kujisomea vitabu na machapisho mbalimbali
hutuwezesha kuwa na uelewa mpana katika maswala mbalimbali yanayoizunguka jamii yetu na ulimwengu kiujumla.
4. Kuhamasisha
waandishi wa Kitanzania hasa katika taaluma ya sheria kwani tuna waandishi wachache sana ambao
wameandika vitabu ukilinganisha na nchi jirani kama vile Kenya na Uganda.
LawAfrica inawakaribisha wale wote wenye nia ya kufanya hivyo kwani kampuni
yetu iko tayari kuchapisha vitabu katika Nyanja ya sheria pasipo mwandishi
kuchangia gharama yoyote.
Kwa awamu
hii ya kwanza jumla ya vyuo kumi na nne (14) kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania vimeweza kunufaika na msaada huu wa vitabu.
Ni malengo
ya kampuni ya LawAfrica kulifanya zoezi
hili kuwa endelevu ili kuweze kufikia vyuo vyote hapa nchini na pia zoezi hili
linafanyika pia katika nchi ya Uganda na Kenya.
TAARIFA HII IMETOLEWA NA:
GWAKISA GEORGE MAKARANGA
MENEJA MKUU WA LAWAFRICA TANZANIA
+255 782 00 44 22
Meneja Mkuu wa Law Africa Tanzania, Gwakisa Makaranga
(wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa Vyuo Vikuu sehemu ya Vitabu
vya Sheria, Mkuu wa Idara ya Sheria Muhadhiri na Mkuu wa Mahakama ya mfano Chuo
Kikuu cha Dodoma,Njiti Batthy,(kushoto) makabidhiano hayo yalifanyika jana Dar
es Salaam,Wengine kutoka kushoto ni Martin Massawe (Chuo kikuu cha
Mzumbe),Rehema Kaunda,(Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam) Anthony Mwenda
(Tumaini Dar es Salaam) Josephine Lawi (Chuo cha Teofilo Dar es Salaam) na
Tumainiel Lyimo wa Chuo cha Sebastian
kolowa Memorial Lushoto.
No comments:
Post a Comment