JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI
YA HABARI NA UHUSIANO
Simu
ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu
ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku
la Posta 9203,
Telex :
41051 DAR
ES SALAAM,12 Septemba,
2013.
Tele
Fax :
2153426
Barua
pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata
habari kupitia mtandao wa Jamii Forum
na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini na waliokuwa
likizo wameitwa kurudi kazini.
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na
Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika
kusonga mbele.
JWTZ linapenda
kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za
upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote.
Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo
kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.
Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya
JWTZ kwenye mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘
(Twitter/ JWTZ).
Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha
na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi
yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji
na zisizo sahihi. Tunapenda
kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.
Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na
kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za
zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu
binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.
No comments:
Post a Comment