Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za
utamaduni wakati alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza
ziara ya kikazi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa
kumbukumbu muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo
kata ya Mondo, Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
bvaadhi ya watoto waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi
Ntulya,katika kata ya Mondo,wilayani Misungwi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisiliza maelezo ya
huduma ya Xray kutoka kwa mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Dr.Marco Mwita
Magessa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua huduma hiyo katika hospitali
ya Wilaya ya Misungwi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto
Paulo Muhangwa muda mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani
Mwanza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na
baadhi ya wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa
huduma ya X Ray katika hospitali hiyo,
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na
mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la Africa School Home Bibi.Aimee Bessire
wakufunua kitambaa katika jiwe lamsingi kuashiria kuzindua rasmi Shule ya
msingi Ntulya.Shule hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Africa School
Home lenye makao yake nchini Marekani.(Picha na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment