Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (wa tatu
kulia), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa wodi ya akina mama na watoto katika
Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki, baada ya kufanyiwa
ukarabati mkubwa na kupatiwa msaada wa vitanda, magodoro, vyandarua pamoja na
mashuka vilivyotolewa na benki ya CRDB. Wa nne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na wa pili kulia Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Baraka Konisaga.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei
akipaka rangi wodi ya akina mama na watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando
jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki. Benki ya CRDB ilikabidhi wodi ya akina mama na
watoto baada ya kuifanyika ukarabati mkubwa, benki hiyo ilikabidhi vitanda,
magodoro, vyandarua vilivyowekwa dawa pamoja na mashuka.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Bungando, Dk. Charles Majinge
akipokea sehemu ya msaada kutoka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo zilizotolewa
na benki ya CRDB kwa ajili ya wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya
Rufaa ya Bugando. Benki hiyo ilikabidhi vitanda, magodoro, blanketi, vyandarua
vilivyowekwa dawa pamoja na mashuka. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyadhiyay.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kusho,to)
akitandika kitanda katika wodi ya akina mama na watoto katika Hospitali ya
Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki baada ya kufanyiwa ukarabati
mkubwa na benki ya CRDB. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki
hiyo, Saugata Bandyadhiyay (kulia) na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa
ya Bugando, Dk. Charles Majinge.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,
Dk. Charles Kimei (wa tatu kushoto) wakimwagilia maji miti ya kumbukumbu walioipanda katika
hospitali ya Rufaa ya Bugando wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya akina mama
na watoto iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na benki CRDB. Hafla hiyo ilifanyika jijini
Mwanza, mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment